Aliyekuwa mpenzi wa Mulamwah, Carrol Sonie yuko tayari kwa mtoto wa pili

Sonie alikuwa anajibu maswali ya mashabiki wake na mmoja alitaka kujua kama anawazia kupata mtoto wa pili.

Muhtasari

• Mama huyo wa mtoto mmoja walitengana na mzazi mwenzake, Mulamwah mwezi Oktoba mwaka jana.

Carrol Sonie, aliyekuwa mpenzi wa Mulamwah
Carrol Sonie, aliyekuwa mpenzi wa Mulamwah
Image: Instagram

Mzazi mwenza wa mchekeshaji Mulamwah, Carrol Sonie amedhibitisha kwamba yuko tayari kupata mtoto wa pili muda mwafaka ukifika.

Akizungumza na mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram kupitia kipindi cha maswali na majibu, Sonie alisema kuwa yuko ana ndoto ya kupata mtoto mwingine, haswa baada ya kutangaza kuwa ameshapata mwanaume mwingine.

“Hello mama K, unaeza taka kupata mtoto mwingine,” shabiki alimuuliza.

“Ndio, wakati muda mwafaka utafika, mbona nisiptate?” Sonie alijibu.

Mama Keilah hivi majuzi alifichua kuwa amepata mpenzi mwingine. Hata hivyo, hakuchapisha uso wake; kwa sababu za wazi. Hakuna uso, hakuna kesi.

Tofauti na Mulamwah, Carrol Sonie amethibitisha kwamba hawezi kuchukua muda mrefu kuchukua nafasi ya ex wake. Ukweli kwamba yeye hachelewi katika kufanya vivyo hivyo unamdhuru zaidi kuliko wema.

Kwa kuzingatia vizazi vyao, Mulamwah na Sonnie hawajawa wazazi wenza kwa amani. Wamekuwa na utengano mbaya ambao umewafanya kufichua siri zao za zamani, ambazo zilipaswa kubaki za siri.

Mulamwah na Sonie waliachana mwishoni mwaka jana na kilichofuatia ni kuchafuliana majina na sifa mitandoni huku wakimvuta hata mtoto wao mchanga Keilah Oyando katika matope hayo.

Baadhi walihisi wawili hao wanamkosea mtoto wao kisaikolojia kwani upo muda atakuja kuwa mtu mzima na kuona jinsi wazazi walikuwa wanarumbana kwa sababu yake, hilo litamuathiri pakubwa sana katika maisha yake ya utu uzima.