Diana Marua akashifiwa kwa kutomsherehekea binti ya Bahati, Mueni

Wanamitandao wamekisia kuwa kuna ugomvi kati ya Diana Bahati na mama Mueni.

Muhtasari

• Bahati alimsherehekea Mueni kwa ujumbe mrefu ila Marua hakuchukua hatua ya kumtakia heri ya kuzaliwa mtoto huyo kama alivyokuwa akifanya hapo awali.

•Hata hivyo, wengine hawakusita kumtetea Marua huku akijaribu kutojihusisha na malalamiko hayo.

Yvette Obura, Mueni Bahati na Diana Marua

Mwanavlogu Diana Marua amekosolewa na baadhi ya wanamitando kwa kukosa kumtakia kheri za kuzaliwa binti ya mume wake Bahati na Yvette Obura, Mueni Bahati.

Bahati alimsherehekea Mueni kwa ujumbe mrefu ila Marua hakuchukua hatua ya kumtakia heri ya kuzaliwa mtoto huyo kama alivyokuwa akifanya hapo awali.

Wanamitandao walitarajia Diana ajiunge na mume wake pamoja na Yvette kumsherehekea Mueni kama walivyofanya mwaka jana.

Kwenye Instagram, mama huyo wa watoto watatu alipakia video na picha zake bila  kumwonyesha Mueni upendo mnamo siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake. Wanamitandao walimkosoa na kumshtumu kwa kutojali.

"Kwa kuwa hayanihusu..wacha nimtakie mtoto mrembo wa kipekee, binti ya Bahati heri ya kuzaliwa,"mwanamtandao aliyejitambulisha kama princesbarbie840 aliandika chini ya chapisho la Diana.

"Sasa hizi ndizo hisia zake za kweli, wakati huo wote ulikuwa kiki. Nyakati hufichua watu wenye nia za kweli. Na pia video aliyofanya na mama Mueni,"kamami.j alisema.

"Hayo ni mambo ya kawaida kabisa. Diana ana roho nzuri, yeye kuwa na upendo mwingi kwa Mueni ni jambo zuri sana. Naomba watatue chochote ambacho kimewatenganisha kwa ajili ya binti huyo,"lavyeen aliandika.

Hata hivyo, wengine hawakusita kumtetea Marua huku akijaribu kutojihusisha na malalamiko hayo.

"Wenye mnalalamika kuhusu Mueni!! Mwacheni Diana Marua!! Wengine wenu mngekuwa kwenye hali yake, hatungewahi kumjua Mueni. Marua alimchukua kama mtoto wake, jambo ambalo wengi wenu hamuezi kufanya ila mnamhukumu! Kile ambacho kimesababisha asimpost hayawahusu!" urscarol alisema.

Kwa upande mwingine, Mama Mueni huku akimsherehekea binti yake, aliwasihi wanamitandao kujiwekea matusi kwani alitaka siku moja tu ya kupumzika ili amsherehekee bintiye.

"Leo zaidi ya siku zote, sijawahi kujaribu hii ila nawasihi mniheshimu na kuwa na maoni yenye heshima. Kuanzia kesho mnaweza kuendelea na chuki au mchiririrzo wa matusi. Niruhusu nimsherehekee mtoto wangu," Yvette alisema.

Wanamitandao wamezidi kushuku kuwa uhusiano wa Diana Bahati na Yvette umekumbwa na changamoto na urafiki wao kudidimia.

Hata hivyo, wote hawajaweka wazi iwapo kuna ugomvi wowote baina yao au sababu ya kutokuwa na uhusiano wa karibu kama hapo awali.