Mobetto avunja kimya kuhusu Diamond kuwa babake mwanawe

Mobetto amewasuta watu wanaosema kuwa mwanawe Dylan si wa Diamond

Muhtasari

• Mobetto alikerwa na madai hayo na kusema kuwa ni mwanamke tu anayefahamu baba ya mtoto wake.

•"Yaani mtoto wangu nyie ndo mumpangie baba?Nyie kama nani haswa?! Binadamu mnapenda sana kujipa mamlaka kwenye maisha ya watu wasiowahusu!" aliendelea.

Hamisa Mobetto na Dylan
Image: Mobetto Instagram

Mwanamuziki wa Tanazania Hamisa Mobetto amemsuta mtangazaji wa radio nchini Tanzania, Mpoki Mjuni kwa kudai kuwa mwana wa kiume wa Mobetto si wa Diamond.

Mpoki alisema mtoto wa Mobetto, Dylan si wa Boss huyo wa WCB bali ni wa mumewe Nandy, Billnass.

Mobetto alikereka na madai hayo na kusema kuwa ni mwanamke tu anayefahamu baba ya mtoto wake.

"Yaani sipendi mtu amzungumzie mtoto wangu!! Sipendi!!Sipendi na sipendi tena jamani. Na wala sijawai elewa watu wazima wanakaaje chini wanaanza kumzungumzia mtoto wa miaka 5 ni kama walikuwepo nikijifungua. Binadamu mkoje nyinyi, au mnataka nini haswaa niwasaidie?!" mama huyo wa watoto wawili aliandika.

Aliwaomba watu kukoma kumhusisha Dylan kwa mambo yake kwani hawajawahi kukutana naye.

Mobetto aliwaambia watu wamzungumzie yeye iwapo wana jambo linalowatatiza kumhusu ila wasimhusishe mwanawe.

"Sidhani kama nimewahi kumuomba mtu yeyote msaada wa kulea watoto wangu. Sipendi kero na mtu na mimi si mtu wa kuropoka, chonde chonde tusije onana wabaya.Yaani mmekosa vya kuongea au ni nini?" mwanamuziki huyo alisema.

"Yaani mtoto wangu nyie ndo mumpangie baba?Nyie kama nani haswa?! Binadamu mnapenda sana kujipa mamlaka kwenye maisha ya watu wasiowahusu!" aliendelea.

Mpoki alikuwa amemzungumzia Mobetto huku akijaribu kuficha jina lake ila alitaja mambo yaliyomhusuisha mwanamuziki huyo.

"Kuna msichana anajulikana sana hapa Tanzania, ana followers wengi, ni zaidi ya milioni 9. Alikuwa video vixen, akapata mtoto wa kiume, ana watoto wawili, wa kwanza wa kike. Kuna jamaa mmoja hapa alitoa wimbo ikavuma sana, naye alikuwa video vixen kwenye huo wimbo. Sasa alipojifungua, hadi kwenye Instagram akaweka jina la huyo jamaa. Jamaa  akakubali, akampa hadi jina, hadi walienda mahakami ," Mpoki alisema.

Alisema kuwa Dylan alifanana na Billnass masikio, mdomo, nyusi na hata macho, bado akijaribu kutofichua jina, alifichua kuwa baba ya mtoto huyo ameoa hivi majuzi.