Nakuwa mgonjwa katika uhusiano sababu naogopa kufanya mapenzi - Akothee

Huwa napenda kupakatwa na kudekezwa, napenda usingizi sana - Akothee aliandika Facebook

Muhtasari

• Siko hospitalini, tulirudi nyumbani and kwa sasa ninaendelea kujihisi vizuri. Ahsante kwa jumbe zenu za kheri njema - Akothee.

Akothee akila bata nono na mpenzi wake mzungu
Akothee akila bata nono na mpenzi wake mzungu
Image: Instagram

Mfanyibiashara ambaye pia ni mwanamuziki Akothee amenyoosha maelezo kuhusu hali yake ya kiafya haswa baada ya awali kuonekana amelazwa hospitalini na mpenzi wake mzungu akiwa anampa uangalizi.

Mjasiriamali huyo amefunguka kuwa alikuwa na matatizo kidogo lakini kwa sasa hayuko tena hospitalini bali walishaondoka humo na mpenzi wake.

Aliwashukuru wafiasi wake na mashabiki wote ambao walisimama naye katika kumtumia jumbe za kumtakia kheri njema na nafuu ya haraka huku akisema kwamba amesharejea nyumbani na anaendelea kujihisi mzima tena.

"Siko hospitalini, tulirudi nyumbani and kwa sasa ninaendelea kujihisi vizuri. Ahsante kwa jumbe zenu za kheri njema," Akothee aliandika kwenye Facebook yake.

Mama huyo wa watoto watano alizidi kuelezea kiini cha ugonjwa wake na kusema kwamba mara nyingi huwa mgonjwa katika uhusiano kwa sababu anaogopa kwa kiasi kikubwa kushiriki tendo la ndoa.

Alisema kuwa mapenzi yake yamo kwa wingi katika kupakatwa kama mtoto na kupetiwa peti huku akisema kwamba yeye anapenda usingizi sana wala hapendi kugeuzwa geuzwa usiku.

Alimalizia kwa kutoa tahadhari kwa wanaume wote ambao wanaweza taka kumchumbia kwamba ni hatari sana, japo onyo yenyewe ilikaa kimzaha zaidi.

"Ninakuwa mgonjwa katika uhusiano kwa sababu naogopa kushiriki mapenzi, huwa napenda kupakatwa na kudekezwa, kazi ngumu ni kupenduliwa penduliwa usiku ugali, sipendi. napenda usingizi, mimi ndio shida. Nichumbie kwa tahadhari yako mwenyewe," Akothee alisema.

Awali, Akothee alionekana amelzwa hospitalini na mpenzi wake mzungu huku akitupa dongo kwa wanaomchukia kuwa walifikiri hangepata mtu wa kumhudumia kwa kumpeleka hospitalini pindi anapougua.