"Nakupenda mubaba wangu" - Nyota Ndogo ampiga busu hadharani Mzungu wake

Alimpokea mzungu huyo aliyerejea nchini na kumpa busu ndani ya treni ya kisasa, SGR.

Muhtasari

• Enyewe mapenzi ni kitu kizuri sana. Nakupenda mubaba wangu,” Nyota Ndogo alimwaga ubuyu wote.

Bw Henning Neilsen na mkewe Nyota Ndogo
Image: INSTAGRAM// NYOTA NDOGO

Msanii mkongwe kutoka Pwani, Nyota Ndogo aefurahia baada ya kumkaribisha mpenzi wake mwenye asili ya Ulaya aliporejea nchini.

Staa huyo wa kibao pendwa cha ‘Watu na Viatu’ alipakia picha akikulana denda na mzungu wake ndani ya gari la moshi la SGR. Alisema kuwa hata hakuamini kufanya kitendo hicho cha faragha hadharani watu wakiwatumbulia macho mchana peupe.

“Nina furaha kukuona umerudi mfalme wangu, karibu nyumbani nilikuwa nimekukosa kinyama hata siamini tumebusiana kwa SGR watu wakituangalia, enyewe mapenzi ni kitu kizuri sana. Nakupenda mubaba wangu,” Nyota Ndogo alimwaga ubuyu wote.

Ndogo na mchumba wake mzungu waligonga vichwa vya habari miaka miwili iliyopita baada ya msanii huyo kuhaha kila kona akililia jicho moja kuwa mpenzi huyo wake alikuwa amemtoroka na kurudi zake Ulaya huku akimblock kwenye mitandao yote ya kijamii.

Alisimulia kuwa alijaribu kumfumba siku ya Wajinga ya Aprili tarehe moja kuwa ana mimba, jambo ambalo Mzungu wa watu alilipokea kwa njia hasi na kumfanya kutumia falsafa ya miguu niponye.

Baada ya kuhaha katika janibu zote, hatimaye aliamua kufungasha safari kuelekea Ulaya ili kumtafuta Mzungu wake na kumuomba samahani kwa mzaha ule wa kuwa na ujauzito wake.

Kweli, alifanikiwa kumkuta na walirudiana na kuwasha mshumaa wa mahaba yao tena ambapo wamekuwa wakivishana koja la maua mitandaoni licha ya kupokea masimango kutoka kwa wanamitandaoni wanaomkejeli Ndogo kuwa anachumbiana na raia wa kigenii mzee, nchini wanamuita ‘Mubaba’