"Natamani angekuwa hapa saa hii!" Mr Seed amkumbuka marehemu baba yake

Msanii huyo alifichua kuwa hakupata nafasi ya kumfahamu vyema mzazi huyo wake.

Muhtasari

•Mr Seed alibainisha kwamba sifa za marehemu ambazo amepata kuskia kutoka kwa watu waliomjua ni nzuri.

•Mr Seed alisema kuwa hiyo ndiyo picha pekee ya wazazi wake pamoja.

Mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za injili na za mapenzi Moses Tarus Omondi almaarufu Mr Seed amemkumbuka marehemu baba yake.

Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa Instagram, Mr Seed alifichua kuwa hakupata nafasi ya kumfahamu vyema mzazi huyo wake.

Mr Seed hata hivyo alibainisha kwamba sifa za marehemu ambazo amepata kuskia kutoka kwa watu waliomjua ni nzuri.

"Sikuwahi kupata wakati mzuri na baba yangu lakini  siku zote naamini kuwa ni alikuwa mtu mzuri. Kwa sababu hiyo sijawahi kuzungumza sana juu yake lakini kulingana na hadithi ambazo nimewahi kuambiwa juu yake, naweza kusema kuwa mwanaume huyo alikuwa akifanya kazi kwa bidii na busara," alisema.

Mtunzi huyo wa kibao 'Only one' aliambatanisha ujumbe huo wake na picha ya marehemu baba yake pamoja na mamake.

Alisema kuwa hiyo ndiyo picha pekee ya wazazi wake pamoja ambayo ako nayo na kueleza jinsi anatamani babake angekuwa hai.

"Natamani angekuwa hapa sahii aweze kuona mtu ambaye nimekuwa. Sasa nasimulia tu kwa watoto wangu hadithi nilizosikia kuhusu yeye. Sijui ata mbona nipost hii lakini nimepost tu ndio muone wazazi wangu ✌️," alisema.

Makumi ya wanamitandao walimiminika chini ya chapisho hilo na kutoa maoni yao kuhusu picha hiyo.  Wengi hawakukosa kutambua mfanano mkubwa kati ya mwanamuziki huyo na mama yake.

@penina_koki Photocopy ya mama

@omari_sammy Mmh unafanana na mama yako

@asispetty Ulichukuwa sura ya mama yote kabisa hiyo siku nikama yeye ndiye alikuwa na nguvu 😂 🙌 lakini inaeleweka kaka 😍 Kama mwana, kama mama.

@esther.mutua Wewe ni kama baba yako yuko mahali pazuri na hakika anafurahi kwa ajili yako mpendwa.