Nililelewa na malkia - Wahu Kagwi ajivunia upendo wa mama yake kwa bintiye

Wahu alisema kuwa ana furaha mama yake akimsaidia kumlea bintiye Shiru

Muhtasari

• Kwenye video hiyo, mamake Wahu, alikuwa mwenye furaha kumbeba mjukuu wake ambaye alikuwa amelala.

Wahu
Image: Wahukagwi Instagram

Mwanamuziki Wahu Kagwi amepakia video ya mamake akiwa amemkumbatia bintiye Shiru ambaye sasa ana takriban miezi miwili.

Kwenye Instagram, Wahu hakusita kuonyesha furaha yake na jinsi anavyojivunia kukuzwa na mama yake.

"Shishi na shosho. Kulea malkia kwa sababu nililelewa na Malkia," Wahu aliandika.

Kwenye video hiyo, mama yake Wahu, alionekana mwenye furaha kumbeba mjukuu wake ambaye alikuwa amelala.

Wahu aliambatanisha video hiyo na wimbo wa 'So Amazing' wa Luther Vandross kuonyesha alivyopendezwa na matukio hayo .

Hivi majuzi, Wahu alikuwa mwenye furaha kwa jinsi binti zake walivyopokea jukumu lao la kumsaidia kulea dada yao mdogo, Shiru.

Alilinganisha jinsi mtoto wake wa pili, Nyakio alikuwa akikumbatia mimba yake kabla ya kujifungua.

Alipakia video mbili katika Instastory zake kuonyesha jinsi binti yake alipenda kuwa na dada mdogo.

"Nyakio alikuwa anakumbatia mimba yangu kila usiku kabla ya kujifungua," Wahu aliandika kwenye video ya kwanza.

Mumewe Wahu, Nameless alifichua kuwa bintiye Shiru alipewa jina la dada yake mkubwa na alieleza furaha yake.

Alisema kuwa bintiye alipewa jina hilo kama tamaduni za Kikuyu.

"Niruhusu nimtambulishe dada yangu Rosemary ambaye Baby Shiru  amepewa jina lake na nina furaha na najivunia kuwa binti yangu wa tatu amepewa jina lake kulingana na mila za Kikuyu," Nameless alisema.

Wapenzi hao wamekuwa wakipakia picha na video ya famili yao ikiwatembelea kumwonyesha upendo mtoto wao mdogo hata kabla atoke hospitalini baada ya kujifungua.