Kajala na Paula ni watapeli, warudishe magari ya Harmonize - Mwijaku

Baba Levo na Mwijaku walisema kuwa Kajala amewablock kila sehemu mitandaoni baada ya kumwambia ukweli kuwa alikuwa anamfyonza Harmonize.

Muhtasari

• Mwijaku alisema hawezi kumuomba radhi Kajala mpaka pale atakaporudisha magari aliyopewa na Harmonize.

• Jumamosi alikuwa ametishia kuenda kumfungulia mashtaka ya kumharibia Harmonize muda.

Mwijaku amkoromea Kajala kurudisha gari la Harmonize
Mwijaku amkoromea Kajala kurudisha gari la Harmonize
Image: Maktaba

Machawa Baba Levo na Mwijaku wamemjia juu Kajala na bintiye Paula kwa kile wanasema kuwa wawili hao walimfyonza kavu msanii Harmonize na kumtoroka mwisho wa siku.

Katika video moja ambayo Baba Llevo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram wakiwa ndani ya gari na Mwijaku, wawili hao walimponda Kajala na kulalama kuwa baada ya kumzomea kwa ukweli wote, Kajala amewapa block wote kila mahali mitandaoni.

Baba Levo alisema kuwa kwa upande wake ameamua kukoma na kumtaka Kajala radhi ila Mwijaku yeye akasisitiza kuwa hawezi kuliacha hilo suala mpaka pale Kajala atakaporudisha magari mawili aliyopewa kama zawadi na Harmonize.

“Hapana, arudishe magari ya watu ndio nimuombe radhi. Rudisha magari kwanza ndio nikuombe radhi. Cha kwanza nimekuta meseji DM, akani’unfollow na kisha kuniblock. Yale magari arudishe,” Mwijaku alisema.

Awali, Mwijaku alikuwa ametishia kuenda kumshtaki Kajala katika kile alisema ni kumharibia muda Harmonize.

“Nakwenda kufungua kesi ya madai mahakamani kesho . Ya kumpotezea muda msanii,” Mwijaku alisema.

Baba Levo naye alisimulia upande wake akisema kuwa Kajala alimfuata DM na kumpa matusi ya nguoni kabla ya kumblock baada yake kumuita Kajala na Paula kuwa watapeli.

“Harmonize tafuta dem mwingine, wale mtu na mama yake ni matapeli, wangekumaliza,” Baba Levo alisema.

Kajala wiki jana alitangaza kuachana na Harmonize pasi na kutoa sababu lakini weney midomo tayari wameshalonga kuwa aliamua kuvunja uhusiano wake na msanii huyo kutoka Konde Gang baada ya kugundua alikuwa amempachika mimba mchepuko.

Harmonize wakati alikuwa anambembeleza Kajala kumrudia, alimrubuni kwa zawadi nyingi yakiwemo magari mawili na zawadi kama mkufu wa thamani kubwa – vitu ambavyo sasa machawa hao wanataka arudishe kwa vile ameshakata mawasiliano na Harmonize.