Ronaldo azawadiwa gari aina ya Rolls Royce yenye thamani ya Ksh 37M na mkewe Georgina

Georgina alipakia zawadi hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na Ronaldo alionekana kwenye video hiyo akitabasamu kwa furaha.

Muhtasari

• Wiki iliyopita, gazeti la Marca liliripoti kwamba Ronaldo 'atasaini' mkataba na Al-Nassr ambao utamweka katika klabu hiyo ya Saudi Arabia hadi 2025.

• Kwa sasa, Ronaldo ni mchezaji huru baada ya Manchester United kuvunja mkataba wake alipofanya mahojiano ya tuhuma kali dhidi ya klabu hiyo.

Ronaldo apewa zawadi ya gari la ifahari na mkewe
Ronaldo apewa zawadi ya gari la ifahari na mkewe
Image: Instagram

Georgina Rodriguez ambaye ni mke wa supastaa wa Ureno Christiano Ronaldo alimnunulia mchezaji huyo gari aina ya Rolls Royce Phantom lenye thamani ya zaidi ya milioni 37 ambazo ni sawa na pauni laki mbili na nusu, kama zawadi ya Krismasi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 kwa sasa yuko kwenye mazungumzo na klabu ya soka ya Saudi Arabia Al-Nassr, na anaripotiwa kukaribia kuafikiana na klabu hiyo kwa pauni milioni 175 kwa mwaka.

Hata hivyo, miongoni mwa harakati za kusaini mkataba mpya, Ronaldo ameonekana kwenye Instagram akitumia muda nyumbani na familia yake.

Georgina alipakia zawadi hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na Ronaldo alionekana kwenye video hiyo akitabasamu kwa furaha kupokezwa zawadi hiyo siku ya Krismasi.

Wiki iliyopita, gazeti la Marca liliripoti kwamba Ronaldo 'atasaini' mkataba na Al-Nassr ambao utamweka katika klabu hiyo ya Saudi Arabia hadi 2025, baada ya kukataa mpango wa kujiunga na klabu hiyo msimu uliopita wa joto.

Inasemekana Ronaldo na familia yake walisalia Dubai hadi dili hilo ambalo pia linatarajiwa kuwa na mikataba kadhaa ya matangazo lilipothibitishwa.

Al-Nassr inachukuliwa kuwa moja ya timu kuu za nchi hiyo, ikiwa imeshinda Saudi Pro League mara tisa, huku taji lao la hivi karibuni likifanyika 2019.

Mshindi huyo wa tuzo maridadi ya Ballon D’or mara 5 kwa sasa ni mchezaji huru baada ya klabu ya Manchester United kuvunja mkataba wao naye baada ya mahojiano makali aliyotoa tuhuma za kutisha dhidi ya klabu hiyo wiki moja tu kuelekea michuano ya kombe la dunia.