"Sijui nini kilitokea kwa kweli," - Rapa wa USA, Meek Mill baada ya kuibiwa Iphone Ghana

Awali msanii huyo alikwa amewasihi walioiba simu hiyo kuirejesha na baadae ilipatikana baada ya wasanii wenza kutoa ombi.

Muhtasari

• Meek Mill alikuwa mmoja wa watumbuizaji katika tamasha la Afro Nations.

Meek Mill
Meek Mill
Image: Instagram

Msanii wa miziki ya Rap kutoka Marekani Meek Mill Alhamisi iliyopita alitangaza kuibiwa simu yake ghali aina ya IPhone na kuwaomba waliomfanyia kitendo hicho kwa wema na huruma kuirudisha.

Msanii huyo alisema kuwa aliibiwa simu hiyo kwa njia tatanishi katika tamasha moja lililokuwa likifanyika nchini Ghana kwa jina Afro Nations.

Mill alilia kwa uchungu akisema kuwa simu hiyo ilikuwa na vitu vingi vya maana kwake na hivyo yoyote ambaye alishiriki katika kuichukua airudishe kwani ilikuwa na takribani nusu ya uhai wake na riziki yake ya muziki pia.

Wasanii wa Ghana wakiongozwa na Shatta Wale walitoa wito kwa aliyeichukua kuirudisha kwa moyo mkunjufu, jambo ambalo baadae lilifanikisha kwani simu hiyo ilipatikana.

Baada ya kuipata, Meek Mill kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika maneno yenye utata akizua kuwa hajui jinsi alivyoibiwa simu hiyo na wala hajui kama mtu aliingia mfukoni ama aliokota ilikoanguka.

Mtu mmoja alishikwa katika tukio hilo lakini Mill alisema kuwa kwa vile hata yeye hajui jinsi simu ilitoweka, hakuwa anataka mtu yeyote kuchukuliwa hatua kwa sababu yake.

“Ningeweza kudondosha simu hiyo kwenye baiskeli ya uchafu ambayo sijui kwa kweli kuna mtu aliingia mfukoni mwangu! Nimerudishiwa hiyo ndiyo niliyohitaji sihitaji mtu yeyote kufungiwa kwa sababu ya simu .., hata sijui ni nini kilitokea,” Meek Mill alisema.