Mchekeshaji Choffuri aibiwa namba ya usajili kutoka kwa gari alilokodisha kupiga misele kijijini

Alisema yeyote ambaye angerudisha namba hiyo angempa shilingi elfu moja.

Muhtasari

• Nilikodisha gari ili niende nipige nalo misele lakini watoto wameling’oa namba ya usajili - Choffuri.

Choffuri alia kung'olewa gari namba za usajili
Choffuri alia kung'olewa gari namba za usajili
Image: Facebook

Mchekeshaji na muigizaji kutoka Magharibi mwa Kenya, Choffuri ni mtu mwenye kutatizika akili baada ya mtu asiyejulikana kung’oa nambari za usajili katika katika gari ambapo alikodisha ili kuenda nalo sherehe za Krismasi nyumbani kwao.

Kulingana na Choffuri, gari hilo alikodishiwa jijini Nairobi ili kupiga misele nalo kijijini mwao katika msimu wa siku ku za Krismasi na mwaka mpya lakini alishangaa kuamka asubuhi moja na kupata gari hilo halina nambari za usajili.

Choffuri sasa Analia akisema kuwa ameshindwa vila ataanza kulirudisha gari hilo kwa mwenyewe likiwa bila utambulisho wa namba ya usajili.

Alitoa wito kwa yeyote ambaye alimfanyia hivo kijijini mwao huku Magharibi mwa Kenya kurudisha namba hiyo ya usajili na kuahidi kumtunuku kwa zawadi nono.

“Nilikodisha gari ili niende nipige nalo misele lakini watoto wameng’oa namba ya usajili. Wanakijiji wenzangu, hili gari si langu, nilikodishiwa na siwezi lirudisha bila namba ya usajili tafadhali. Mwenye alichukua nirudishieni tu nitalipa elfu moja,” Choffuri mwenye mawazo yaliyotatizana alisema kwa uchngu.

Katika mahojiano ya kipekee kupitia simu na Radio Jambo, Choffuri ambaye ni mchekeshaji wa kwanza kutoka jamii ya Abaluhya kufanya maudhui ya mitandaoni alisema kuwa bado hajapata kurudishiwa namba hiyo na kusema tayari amemtaarifu mwenye gari kuhusu kisa hicho.

"Sijapata bado, lakini nimemuelezea mwenye gari. Nikamuambia kama itapatikana ni sawa na isipopatikana nitamlipa aendee nyingine," alisema.