Jackie Matubia afichua kwa nini anachukua mapumziko kwenye mitandao ya kijamii

"Je, utawaambia ukweli? kwamba hufanyi hivyo kwa sababu ulijaribu na haikufanya kazi"

Muhtasari
  • Hii ni kumsaidia kuzingatia mradi fulani mkubwa anaofanyia kazi ambao unahitaji kujitolea kwake kamili
Image: INSTAGRAM/ JACKIE MUTUBIA

Jackie Matubia atakuwa nje ya mtandao wa kijamii kwa wiki kadhaa.

Hii ni  ili kumsaidia kuangazia mradi fulani mkubwa anaofanyia kazi ambao unahitaji kujitolea kwake kamili.

Kupitia chaneli yake ya youtube, Jackie aliwaambia mashabiki anahitaji muda wa kujitenga ili kufanikisha mradi ambao ameweka malengo yake.

Kulingana na maelezo aliyofichua kwenye youtube, Jackie amekuwa akikabiliana na hali ya kufadhaika kuhusu jambo hilo na hataweza kutenga muda zaidi kuifanya.

"Salamu kwa kila mtu anayesukuma kuniamini, cha kuchekesha ni kuwa inaweza kuonekana kama mambo hayatokani kwangu, inaweza kuonekana kuwa kuna dhoruba kwangu kama hivi sasa niko kwenye dhoruba na ninahisi kama nimefanya hii lakini kuna kitu kinanipiga, unajua,"

Akigeukia upande wa Blessings Jackie alisema,

"Unajua kama mwaka jana kwangu kuna kitu kilikuja, nahisi kama vitu,  lakini nilijiambia nikikaa hapa kitandani na kulia na kuvunjika chini na kuwa na hisia kwa kila mtu na kutotaka kuzungumza na mtu yeyote hakuna kitakachobadilika"

Aliongeza;

"Bado nitaamka siku inayofuata na bado nina shida kama hiyo, lakini nifanye nini sasa"

Blessing anasema Jackie alijaribu kufanya kazi kwenye mradi huo bila mafanikio.

"Je, utawaambia ukweli? kwamba hufanyi hivyo kwa sababu ulijaribu na haikufanya kazi"

Jackie anakubali kuwa "kwa wiki nzima nilikuwa nalia naamka bado ni vile vile, kwanza ni mbaya zaidi" Blessing alimkiri Jackie kuwa mwanzoni alikuwa hajui anachopitia lakini anajivunia jinsi alivyomudu.

"Unapoona mtu anatoka kwenye hiyo unaona ni nguvu kiasi gani inatakiwa coz siwezi kukutoa inabidi upate nguvu ya kutoka na ninashukuru na kujivunia wewe"