Na hili jumba lote, mume wangu anataka watoto 2 tu - Lady Risper

"Nani atamwambia waluhya tunapenda kuzaa,” Lady Risper alisema.

Muhtasari

• Brian na Risper walikutana mtandaoni na kuoana miaka iliyopita. Wawili hao wana mtoto wa kiume pamoja.

Lady Risper aonesha jumba lake la kifahari
Lady Risper aonesha jumba lake la kifahari
Image: Instagram

Mwanasosholaiti mstaafu Lady Risper kwa mara ya kwanza ameonehsa picha ya muonekano wa jumba lake na mume wake huku akizua utani kwamba na ukumbwa wa jumba hilo bado mume wake anataka wazae tu watoto wawili pekee.

Jumba hilo la kifahari lenye urefu wa ghorofa mbili na vyumba kadhaa Ripser alisema ni boma lake ambalo wanaishi na mume wake huku akitaka watu wamshauri mume wake kuwa Waluhya, yeye akiwa mmoja wao wanapenda kuzaa watoto wengi kwa hiyo hafai kumwekea ukomo.

“Pamoja na vyumba vyote hivi na bado mume wangu anataka watoto 2 tu,nani atamwambia waluhya tunapenda kuzaa,” Lady Risper alisema.

Mwanasosholaiti huyo mwenye muonekano wa aina yake ameolewa na mwanaume kwa jina Brian Muiruri ambaye si mzungumzaji sana.

Kando na kuwa na jum a zuri la kifahari lenye hadhi ya nyota tano, Brian aliripotiwa kuachana na Risper mnamo mwezi Septemba mwaka jana lakini akambembeleza kwa kumnunulia mwanasosholaiti huyo gari kama msamaha.

Risper alipokea gari hilo na kusema kuwa amekubali kupokea msamaha wa mumewe na kurudiana naye.

Brian na Risper walikutana mtandaoni na kuoana miaka iliyopita. Wawili hao wana mtoto wa kiume pamoja.

Baadhi ya mashabiki wake walimhongera kwa jumba zuri huku wengine wakijitolea kupewa nafasi ya kumzungumzia mumewe ili abadili fikira zake kuhusu kupata watoto wawili tu.

Mimi Naeza kukusaidia kumshawishi.😆Kama  Mluhyia halali mwenye watoto wane na wote wakati mwanaume wangu alikuwa anataka watoto kumi, niliishia kwa wane tu,” mmoja kwa jina Bee Maube alisema.

Wengine walimwambia pengine anahitaji wawili tu kutoka kwake na kuongeza wengine kutoka kwa wanawake wengine.