Kuita mtu mwenye ufanisi akiwa mdogo G.O.A.T ni ushetani - Pastor T Mwangi

"Ukiangalia asili ya GOAT, unaona kuwa sura ya shetani inawakilishwa na pampati, mtu mwenye kichwa cha mbuzi na vidole vikinyoohwa juu." - T alisema.

Muhtasari

• T alifafanua zaidi kuwa historia ya GOAT ilianzia Ugiriki kwa Alexender The Great.

• Aidha alisema kuwa si vibaya kwa mtu kupata mafanikio akiwa mdogo.

Mchungaji T Mwangi akionya kuhusu GOAT.
Mchungaji T Mwangi akionya kuhusu GOAT.
Image: INSTAGRAM

Mchungaji wa kanisa la Life Church International lililoko Limuru kaunti ya Kiambu, T Mwangi amewasuta vikali wale wanaotumia jina la GOAT kwa watu ambao wamefanikiwa katika maisha.

Kulingana na mchungaji huyo mweney mafunzo yenye misimamo mikali dhidi ya ushirikina na ushetani, kuita mtu kwa jina GOAT ni ushetani, huku akisema kuwa huo ni mfano wa kinyago cha kishetani cheney kichwa cha mbuzi na mwili wa binadamu na ambacho kilikuwa kinaabudiwa na baadhi ya madhehebu ya kishetani.

Akifafanua zaidi kupitia TikTok, T Mwangi alisema kuwa kuita watu waliofanikiwa na umri mbichi GOAT kumekataliwa katika kitabu cha Daniel 8:9 ambapo pia alifafanua zaidi kuhusu historia ya Alexender The Great wa kwanza aliyetawala Ugiriki akiwa mdogo na kupata mafanikio makubwa.

T alisema kuwa kiongozi huyo wa enzi za zamani za Wagiriki alikuwa anaamini katika kinyago chenye kichwa cha mbuzi na mwili wa binadamu na ndio akaanza kuitwa GOAT.

Hata hivyo, Mwangi alisema kuwa si vibaya kwa mtu kupata mafanikio makubwa maishani akiwa mdogo na kusisitiza kuwa alichokuwa akikikataa ni kumuita mtu kama huyo GOAT.

“Alexender alikuwa kiongozi mkubwa aliyefariki na miaka 32. Wakati watu walikuwa wanazungumzia GOAT, walikuwa wanamzungumzia kijana huyo ambaye alifanya makubwa akiwa na miaka chini ya 32 tu. Lakini pia ukiangalia asili ya GOAT,, unaona kuwa sura ya shetani inawakilishwa na pampati, mtu mwenye kichwa cha mbuzi na vidole vyake kwa ishara inayoelekeza mbinguni. Kwa hiyo, kunaweza kuwa na uhusiano na ushawishi wa kishetani na watu wanaosukuma jina la GOAT mbali zaidi,” Mchungaji T alisema.

Katika dunia ya sasa, haswa katika malimwengu ya spoti, watu mbalimbali wamebandikwa majina ya GOAT kutokana na ufanisi wao mkubwa katika vitengo mbalimbali vya michezo.

Miongoni mwa nyota wa michezo waliopewa jina hili ni pamoja na Christiano Ronaldo, Lionel Messi, Serena Williams wa tenisi, Usain Bolt wa riadha kutoka Jamaica, Eliud Kipchoge wa Kenya kati ya makumi ya wengine.