Mimi si mke wako na siwezi kuwa rafiki yako, nitakuanika! - Anerlisa kwa Ben Pol

"Unajua vizuri sana kuwa nikiamua kufanya mahojiano kuweka mambo wazi, sijui utaficha uso wako wapi?" Anerlisa alimuuliza Ben Pol.

Muhtasari

• Anerlisa alidokeza kuwa ni mengi ambayo ameamua kunyamazia kutoka kwa msanii huyo na siku ataamua kuyaweka wazi mitandao ya kijamii itamcheka.

Anerlisa Amshtum vikali Ben Pol
Anerlisa Amshtum vikali Ben Pol
Image: Instagram

Mjasiriamali na mrithi wa kampuni ya vileo ya Keroche Anerlisa Muigai amemtaka mwanamuziki Ben Pol kusonga mbele na maisha yake bila kukwama kweney matumaini kuwa siku moja watarudiana.

Muigai kupitia ukurasa wake wa Instagram, alisema kuwa kufuatia madai ya hivi juzi ya msanii huyo kuhusu kutofurahi uhusiano wao enzi wakiwa wanandoa, alitaka kumjibu kwa kufanya mahojiano na vyombo vya habari na mablogu lakini baada ya tathmini ya muda aliona haina haja.

Alitoa tamko kali kwa Pol akimkumbusha kuwa imekuwa miaka miwili tangu watengane na kuvunja uhusiano wao, hivyo wao si marafiki tena na hakutakuja kutokea siku wanarudiana.

Alimtaka msanii huyo kukoma mumzungumzia katika mahojiano yake ya badala yake kujishughulisha na maisha yake huku akifichua kuwa ni mengi ameamua kuyaficha na siku akifunguka kwa vyombo vya habari hajui Ben Pol ataficha uso wake wapi.

“Baada ya kupiga hesabu ndefu na kufikiria kwa kina, nimeona hakuna haja nifanye mahojiano kumjibu Ben Pol kuhusu uhusiano wangu wa awali na yeye.  Niligundua kuwa haistahili muda wangu kabisa kulizungumzia hilo kwa sababu sasa hivi mimi ni bora kuliko muda huo.”

Alimtaka kuondoka fikira ya kurudiana, kitu ambacho alikitaja kuwa huenda msanii huyo amekuwa akimbembeleza faraghani na ameweka wazi haliwezi tokea kwani tayari maji yalishamwagika.

“Lakini kwa kumkumbusha tu Ben, ni miaka miwili sasa tangu tutengane. Mimi si mke wako na ni wazi pia kuwa siwezi kuwa rafiki yako. Songa mbele na maisha yako na koma kudhani kuwa tutakuja kurudiana. Haiwezi tokea. Unajua vizuri sana kuwa nikiamua kufanya mahojiano kuweka mambo wazi, sijui utaficha uso wako wapi,” Anerlisa Muigai alifoka.

Mwishoni mwa wiki jana, mahojiano ya Ben Pol akizungumzia uhusiano wake na Anerlisa huku akisema kuwa hakuwahi furahia hata kidogo yalivujishwa na kuzua gumzo kali mitandaoni.

Anerlisa alimshauri kuwa kama hataki amuaibishe basi ni vizuri aliweke jina lake mbali na mdomo wake na asijaribu kulitumia kama njia ya kusukuma mziki wake.

"Kwa hiyo kukuepushia aibu, weka jina langu mbali na mdomo wako, usijaribu kulitumia kusukuma kazi zako za muziki, kama umeshindwa na muziki tafuta kazi ama urudi shule," Anerlisa alisema.

Ben Pol na Anerlisa walifunga ndoa ya kanisani mwaka 2021 na kuachana miezi michache baadae, jambo ambalo lilisemekana kumsukuma msanii huyo kupatwa na msongo wa mawazo na hata kudaiwa kubadili dini kutoka Ukristu hadi Uislamu.