Vijana, haijalishi babako amefanya nini, kumpiga hakufai kabisa - Robert Burale

Alisema alichukizwa sana na video moja aliyoona vijana wakimpiga baba yao.

Muhtasari

• Vijana haijalishi baba yako amefanya nini ..kumpiga baba yako ni hapana - Burale alisema.

Robert Burale ashauri vijana kutopiga baba zao
Robert Burale ashauri vijana kutopiga baba zao
Image: Facebook

Mtaalam wa masuala ya ndoa na ji nsi ya kuishi vizuri Robert Burale ameonesha ghadhabu yake kwa vijana ambao wanawaadhibu baba zao kwa kuwachapa viboko na makofi.

Burale alisimulia kupitia ukurasa wake wa facebook akisema rafiki yake alimtumia video moja vijana wakimchapa baba yao – video ambayo japo hakuionesha lakini aliielezea kama ya kuchukiza na kuchefua moyo vibaya.

Aliwashauri vijana kuwa haijalishi baba mzazi amekosea nini au anajibeba kwa njia gani, lakini hatua ya kumuadhibu kwa kumchapa haifai kufikiriwa hata kidogo.

“Rafiki yangu alinitumia video ya baadhi ya vijana wakimpiga baba yao...Kuna mgogoro...Kuna haja ya dharura ya kuwaokoa wanaume..Kukosa ushauri kumesababisha matatizo makubwa...Vijana. .haijalishi baba yako amefanya nini ..kumpiga baba yako ni hapana... Mtu mmoja kwa wakati mmoja .... Tutafika huko na Kurudisha heshima kwa Utu uzima,” Burale alisema.

Wengine wlaimlaumu pia yule aliyechukua video ile wakisema kuwa asingefanya vile bali angechukua jukumu la kuwakanya vijana wale kuwa walichokuwa wakifanya sicho.

“Kuchukua video inapaswa kuwa hapana. Mtu wa kamera anahitaji somo pia,” Peter Tirop alisema.

“Kibiblia haikubaliki hata kwa mwanaume kumdharau baba yake bila kujali mazingira. Baba atabaki kuwa baba daima,” mwingine alisema.

Burale ambaye pia anajingeza kama mchungaji alisema ni wakati sasa vijana waanze kupewa ushauri nasaha jinsi ya kuwaheshimu wazazi haswa kina baba ambao katika miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakipitia madhira mengi ambayo hayazungumziwi hadharani.