Betty Kyallo aenda kisheria zaidi kushughulikia uvumi wa kuvujishwa kwa picha za utupu wake

Kampuni ya Medios inayosimamia kazi za Kyallo ilisema tayari imetoa malalamishi yao kwa DCI na kuhakikishiwa kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa.

Muhtasari

• "Asili ya maudhui yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni ghushi, ni mbaya na yenye nia ya kuchafua chapa ya Betty Kyallo" taarifa hiyo ilisoma kwa sehemu.

Mwanahabari Betty Kyallo
Mwanahabari Betty Kyallo
Image: INSTAGRAM

Medios, kampuni inayosimamia brand ya mwanahabari Betty Kyallo imekanusha vikali madai yaliyokuwa yakienezwa mitandaoni kuwa picha na video za utupu za mwanahabari huyo zimevujishwa.

Katika taarifa ambayo Medios waliitoa kwa umma, walikanusha madai hayo huku wakitoa onyo kali kwa wale ambao wanajaribu kueneza habari hizo za uongo wakitumia jina la mteja wao.

“Tumejulishwa kwamba kuna hadithi ya uongo inayoenezwa mitandaoni kwamba mwanahabari na mfanyibiashara Betty Kyalo ameshiriki katika kuzalisha video chafu. Tunachukua fursa hii kukanusha vikali na kukashfu hadithi hizo ghushi zinazoenea na kuhusisha jina la Kyallo,” Medios walisema.

Walijitambulisha kama kampuni inayowakilisha Betty Kyallo katika shughuli zake za kibiashara na kisheria pia.

Walisema tayari wametoa taarifa rasmi ya malalamishi kwa DCI ili kuanzisha uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yule aliyeanzisha hadithi hizo feki.

“Asili ya maudhui yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni ghushi, ni mbaya na yenye nia ya kuchafua chapa ya Betty Kyallo ambayo kwa muongo mmoja uliopita imekuzwa kwa maadili makubwa. Tayari tumetoa barua ya malalamishi rasmi kwa kitengo cha DCI na tumepata hakikisho kwamba blogu au chombo cha bahari au mtu yeyote aliyeanzisha uvumi huo atashtakiwa,” Medios ilitamka.

Awali mwanahabari huyo alikuwa atazungumziwa sana kwenye mitandao ya kijamii za ndani zikisema kuwa kuna mahali picha za utupu wake zilionekana lakini taarifa hiyo haikuchukuliwa kwa umakini na wengi.

Kyallo mwenyewe katika instastoy yake kabla ya kuifuta, alishangaa kuwa ameshtukia akiambiwa anatrend ila akapuuza na kusema kuwa yeye fikra zake zote zilikuwa katika kazi zake.