Burna Boy, Davido na Wizkid wang'ara tuzo za Afrima

Burna Boy, Davido na Wizkid walitawala tuzo za nane za All Africa Music Awards (Afrima).

Muhtasari

•Tala wa msanii wa Ivory Coast Didi B, umetajwa kuwa wimbo bora wa mwaka katika sherehe ya kifahari iliyofanyika katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

•Burna Boy, Wizkid na Davido hawakuonekana kwenye sherehe za kupokea tuzo zao.

Burna Boy
Image: BBC

Mastaa wa muziki wa Nigeria kama vile Burna Boy, Davido na Wizkid wametawala tuzo za nane za All Africa Music Awards (Afrima).

Tala wa msanii wa Ivory Coast Didi B, umetajwa kuwa wimbo bora wa mwaka katika sherehe ya kifahari iliyofanyika katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Mwaka huu mastaa wakubwa wakiwemo rapper wa Ghana Black Sherif na ndugu wa Nigerian P-Squared walipanda jukwaani kutumbuiza.

Mwimbaji wa Nigeria Asake alitangazwa kuwa Mwanamuziki Bora wa Mwaka wa 'aliyetoka'. Wakati wa hotuba yake Asake, ambaye jina lake halisi ni Ahmed Ololade, alisema kushinda tuzo hiyo ni ndoto iliyotimia: "Ilianza kama ndoto, lakini leo, ni ukweli. Asante kwa Mungu, lebo yangu na mashabiki wangu wote wanaosikiliza nyimbo zangu."

Burna Boy, aliyeshinda tuzo ya Msanii Bora wa Mwaka na Albamu Bora ya Mwaka, Davido, aliyeshinda Msanii Bora wa Kiume katika Muziki wa Inspirational Afrika, na Wizkid, aliyeshinda tuzo ya msanii bora wa Afrika, hawakuonekana kwenye sherehe za kupokea tuzo zao.

Kulikuwa na utata katika maandalizi ya tuzo hizo, baada ya watu kutia saini ombi la kumtaka mwimbaji wa Nigeria Brymo asishinde tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka, baada ya kutuma mfululizo wa ujumbe kwenye mtandao wa twitter zilizotafririka kama matusi kuhusu kabila la Igbo la Nigeria.

Zaidi ya watu 40,000 walitia saini ombi hilo dhidi ya mwimbaji huyo, ambaye jina lake halisi ni Olawale Ashimi.