Nimeumia sana-Otile Brown aeleza jinsi alivyoibiwa kwenye uwanja wa ndege Tanzania

Otile ametilia shaka kiini cha walinzi ikiwa hawawezi kusaidia inapohitajika zaidi.

Muhtasari
  • Mwanamuziki huyo wa Kenya hata hivyo hakufichua thamani ya vifaa vyake vya kielektroniki ambavyo vimetoweka katika uwanja wa ndege
Msanii wa kizazi kipya Otile Brown katika mahojiano ndani ya rdio Jambo.
Msanii wa kizazi kipya Otile Brown katika mahojiano ndani ya rdio Jambo.
Image: Radio Jambo (Facebook)

Mwimbaji wa R&B Otile Brown amechanganyikiwa baada ya kupoteza kompyuta zake mbili za mkononi nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Mwanamuziki huyo wa Kenya hata hivyo hakufichua thamani ya vifaa vyake vya kielektroniki ambavyo vimetoweka katika uwanja wa ndege.

"So kwenye airport ya Julius Nyerere Tanzania nimeibiwa Mac/laptop mbili ila walinzi nawatoa huduma wamekataa kutusaidia ndani ya masaa matatu. Wamektaa kuangalia kwenya cctv. Wametungusha mda. Usiku mrefu zaidi wa maisha yangu.

Yani wanakataa kutoa huduma wakati ku trace laptop zikiwa tu hapo karibu. Tumetoa hadi report ya police ambayo ndio utaratibu ila wakakataa.

Otile ametilia shaka kiini cha walinzi ikiwa hawawezi kusaidia inapohitajika zaidi.

Kwani security kazi yake ni gani kama hawawezi kukusaidia? Mimi kama mpenzi wa nchi ya Tanzania nimeumia sana. I need a lawyer. I would have retrieved the laptops tonight, but it's like they wanted us to lose them. Sad.