Ombi la Charlene Ruto kwa vijana baada ya kuadhimisha miaka 30

Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii, alisema atashiriki maoni 30 bora katika siku zijazo.

Muhtasari
  • Binti ya rais amekuwa akiwashirikisha vijana kikamilifu kupitia mipango mbalimbali na programu za kuwafikia
CHARLENE RUTO
Image: CHARLENE RUTO/TWITTER

Binti ya Rais William Ruto Charlene Ruto alisherehekea siku yake ya kuzaliwa wiki jana Januari, 11, 2023 akiwa na marafiki na familia wa karibu.

Siku chache baada ya kushiriki wakati huo na wapendwa wake, Charlene alisema anataka kuendeleza sherehe hiyo kwa vijana wa Kenya, na akawataka kupendekeza njia ambazo wangependa kushiriki.

Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii, alisema atashiriki maoni 30 bora katika siku zijazo.

Binti ya rais amekuwa akiwashirikisha vijana kikamilifu kupitia mipango mbalimbali na programu za kuwafikia.

"Jumatano iliyopita, hatimaye nilijiunga na ghorofa ya 3 na kufikisha mwaka mmoja zaidi. Kwa miaka yangu ya 30, ningependa kupata maarifa kutoka kwa Vijana wa Kenya.

Tafadhali toa maoni yako au tuma DM juu ya mambo 30 ambayo tunaweza kufanya kazi pamoja mwaka huu ili kuongeza thamani kwa nchi yetu. Tutashiriki 30 bora wiki ijayo, "chapisho hilo lilisoma.

Wakati wa sherehe zake za faragha, bintiye rais alimwagiwa zawadi zikiwemo keki mbili na mashada ya maua.