Baba Levo njia panda aliyekuwa mkewe akimuomba msamaha na kutaka warudiane

Mkewe ambaye walikaa kweney ndoa kwa miaka 7 alitoroka na sasa amefunguka kuwa marafiki wabaya ndio walimshauri.

Muhtasari

• Baba Levo ambaye tayari alishadokeza kuwa na uhusiano na mwanamke mwingine Mturuki alisema yuko kwenye njia panda kuhusu kurudi au kuendelea na mzungu wake.

Baba Levo achanganyikiwa kumrudia mke wake
Baba Levo achanganyikiwa kumrudia mke wake
Image: Instagram

Mkewe msanii na chawa wa Diamond Platnumz Baba Levo aliyeitoroka ndoa yake mwezi Agosti mwaka jana ameomba msamaha kwa Levo na kutaka warudiane.

Mwanamke huyo kwa jina Salma au mama Ruby alisema alidanganywa na watu ambao walimpa ushauri wa kumpotosha na kufanikiwa kumtoa kabisa katika ndoa yake.

Salma ambaye alipakia video kwenye Instagram alimuomba Levo msamaha huku akisema kuwa amegundua thamani yake kama mke imekuwa ikishuka tangu aitoroke ndoa yake.

“Tumeishi ndani ya miaka saba lakini hapa katikati kilitokea kitu ambacho niseme sijui ni shetani kwa sababu marafiki ambao hawakuwa na nia nzuri na ndoa yetu walitutenganisha kwa kunishauri na kujijaza kichwa kuona kwamba kukaa ndani ya familia yangu ni ujinga."

"Nimegundua kuwa thamani niliyokuwa nikiipata ndani ya ndoa sio ambayo naipata nikiwa nje. Natumia ukurasa huu kuomba radhi kwa mume wangu kipenzi. Sasa hivi nahitaji kwa kweli kuwalea watoto wangu katika familia,” alisema Salma.

Pia alitumia nafasi hiyo kutoa ushauri kwa wanawake wengine kutokubali ushauri kutoka kwa watu wanaolenga kuwatenganisha na wapenzi wao.

Kwa upande wake, Baba Levo kupitia Instagram yake alidhihirisha kuwa huenda amekubali kumsamehe na alimjibu kwa kuweka picha akiwa na mrembo kutoka Uturuki.

Nauona Mtihani Uliopo Mbele Yangu…!! Ila Naamini Ntavuka Salama …!! Naheshimu Ujasiri Wa Mama Ruby Ana Stahili MSAMAHA Naamini Amejifunza Vya Kutosha Na Kwa Sasa Atakuwa Mke Mwema…!! Ni Muda Wangu Wa Kumuomba Msamaha Mzungu ..! ! Najua Hatofurahishwa Na Hizi Taarifa,” Baba Levo alidokeza kurudi kwa mke wake.

Wasanii mbalimbali walimshauri kuchukua ushauri wa kurudi kwa mke wake huku wengine wakimwambia kuwa mambo ya Mzungu kutoka Uturuki hatowezana naye.

“Rudi kwa mkeo mwenzangu mambo ya kurudi nyumbani umechoka afu uanze kuongea kingereza yanachosha nayo,” Zuchu alimwambia.

“Sisi Tunampenda Mama Rubby we Rudi Tuu atakutajia wote waliomshawish😂😂 Daah” mwigizaji mkongwe Wolper alisema.