Jackie Matubia: Tulikutana na Blessing mara ya kwanza kwenye mahojiano ya TV

"Mimi nilisema yeye ni mwigizaji na nilikuwa namtambulisha. Hicho ndicho kitu cha kwanza nilimwambia,” - Matubia.

Muhtasari

• Wawili hao walipoondoka katika kipindi cha Zora kilipotamatika, walioana na mpaka sasa wana mtoto pamoja.

Jackie Matubia na Blessing Lungaho,
Jackie Matubia na Blessing Lungaho,
Image: instagram,

Mwigizaji Jackie Matubia amefunguka ukweli wake mahali walikutana na mpenzi wake ambaye pia ni mwigizaji Blessing Lungaho na kile alichosema mara ya kwanza walipokutana miaka michache iliyopita.

Kupitia blogu yao ya YouTube, Matubia alisema kuwa kwa mara ya kwanza walikutana na Lungaho ni katika mtaa wa South B ambapo kila mmoja alikuwa ameenda kuhudhuria mahojiano ya runinga.

“Mara ya kwanza nilimkuta Blessing ni kwa mahojiano ya runinga South B eneo la Boma Inn. Mimi nilisema yeye ni mwigizaji na nilikuwa namtambulisha. Hicho ndicho kitu cha kwanza nilimwambia,” Matubia alisema.

Kwa upande wake, Blessing japo alikubali hapo ndipo walikutana kwa mara ya kwanza, ila alitofautiana na kile ambacho alimwambia kwa mara ya kwanza.

Kulingana na yeye, kitu cha kwanza Matubia alimtamkia ni “karibu” huku naye akijibu “ahsante”

Mwigizaji huyo alisema kuwa Blessing Lung’aho hana chaguo la sehemu nzuri ambayo anaweza pendekeza kwa ajili ya kutembelea bali yeye muda wote husema sehemu yoyote ambapo kuna kitanda ni sawa.

Wengi wamekuwa wakijua kuwa wawili hao waliutana katika mfululizo wa filamu ya Zora ambayo ilikamilika miaka miwili iliyopita ambapo wote walikuwa wanashiriki kama waigizaji.

 Kipindi hicho kilikuwa kinapepereshwa kwenye runinga ya Citizen. Baada ya kukamilika kwa kipindi hicho, wawili hao waliendeleza uhusiano wao na kuupeleka katika kiwango kingine walipotangaza kutarajia mtoto pamoja.