Msanii B Classic amtaka Shakilla kuwa mcha Mungu ili amfanye mke wake

Shakilla alikuwa ameonesha wasiwasi wake kuhusu ni kwa nini hapati mwanamume wa kumtongoza.

Muhtasari

• B Classic alisema pia yuko mbioni kutafuta mwanamke mcha Mungu ili kutulia katika ndoa na yeye.

• Shakilla ambaye amekuwa akionesha dalili zote za mtu anayeshambuliwa na msongo wa mawazo, alisema ana mashaka kuwa hatongozwi.

B Classic ammezea mate Shakilla
B Classic ammezea mate Shakilla
Image: Instagram

Mwanamuziki kutoka pwani ya Kenya, B Classic 006 ametangaza kuwa tayari kumchukua mwanasosholaiti Shakilla kama mke wake.

Hili linakuja siku chache tu baada ya Shakilla kuonesha wasiwasi wake kuwa hakuna mwanamume wa maana anayejaribu kumtongoza wala kutaka ndio yake katika ndoa.

Shakilla alisema kuwa licha ya kuwa na wafuasi wengi zaidi la laki 3 kwenye mtandao wa Instagram, hakuna hata mwanamume mmoja amejaribu kufanya udhubutu wa kumtongza, jambo ambalo limempa msongo wa mawazo akijiuliza maswali iwapo yeye aliumbwa makusudi kwa ajili ya mitaa na si kutulia kwa boma na mume wake.

“Kwa hiyo tuseme katika wanaume wote ambao wananifuata Instagram hakuna hata mmoja anayetaka kuingia katika uhusiano wa hakika na mimi. Kwani mimi nilikusudiwa kuwa wa mitaani katika maisha yangu yote bila familia?” Mwanasosholaiti huyo aliuliza kwa wasiwasi mkubwa.

Baada ya kuona hili, mwanamuziki B Classic amejitolea kuwa mwanamume wa kipekee kumuondolea aibu Shakilla kwa kumchukua na kumweka ndani kama mke wake.

Lakini hilo haliji bur tu, B Classic alitoa kigezo ambacho huenda kikawa kigumu kwa Shakilla kukubali ili kuwa mke wake.

Msanii huyo alimtaka Mwanasosholaiti Shakilla kukubali posa yake iwapo ako tayari kubadili tabia na mienendo yake na kuwa mwanamke mcha Mungu ambaye atakuwa anatumia muda wake mwingi kanisani kusujudu.

“Shakilla nimeona pia uko soko kama mimi, naweza nikakuoa na nikakupa maisha mazuri tu. Ila, uko tayari kubadilika? Naweza kusimamia kwa kila kitu. Bora tu nione unakuwa mtoto wa kanisani haijalishi itakuchukua muda mrefu kiasi gani. Kama uko tayari nitakuwa na faraja sana, DM yangu iko wazi,” mwanamuziki huyo alisema.

Ila asilimia kubwa ya wanamitandao ambao wamekuwa wakimfuatilia kwa ukaribu Shakilla wanaamini kuwa hiki kigezo cha kuwa mtoto wa kanisani kitakuwa kibarua kigumu kwa kiasi cha haja kwa mwanasosholaiti huyo.

Kwa kwa kuangazia upande wa pili wa sarafu, hakuna gumu linalishindikana chini ya jua pakiwepo nia, ari na uchu!