Msanii Rayvanny ampoteza kaka yake-Baba Levo afichua

"POLE SANA MDOGO WANGU @rayvanny KWA KUONDOKEWA NA KAKA YAKO…!MUNGU AKUPE NGUVU

Muhtasari
  • Kulingana na chapisho lililosambazwa na mtangazaji wa redio ya Wasafi, Baba Levo, kwenye akaunti yake rasmi ya Instagram, mwanamuziki huyo kwa sasa anaomboleza kifo cha kaka yake
Rayvanny ajitosa siasani
Rayvanny ajitosa siasani
Image: TikTok

Staa wa bongo kutoka Tanzania Rayvanny amempoteza kaka yake.Habari hizi zilifichuliwa na mtangazaji wa Wasafi Babalevo.

Kulingana na chapisho lililosambazwa na mtangazaji wa redio ya Wasafi, Baba Levo, kwenye akaunti yake rasmi ya Instagram, mwanamuziki huyo kwa sasa anaomboleza kifo cha kaka yake.

Baba Levo ambaye pia ni mwanamuziki na rafiki wa karibu wa Rayvanny, alitumia akaunti yake ya Instagram kumpa pole mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu sana.

"POLE SANA MDOGO WANGU @rayvanny KWA KUONDOKEWA NA KAKA YAKO…!MUNGU AKUPE NGUVU KWENYE KIPINDI HICHI KIGUMU🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼,"Aliandika BabaLevo.

Mashabiki walitoa pole zao kwa msanii huyo na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

mbeyadreadlocks_clinic: Pole sana rayvnny mungu akutie nguvu sana

kakole_de_santox: Duuuh 😢😢 pole ndugu yetu

amodaneissaamir: Pole rayvanny mungu akupe nguvu kwenye kipindi hichi😢

fatuma_machemba: Mm nilisema wanagombana ndugu huu uchimbii (uchuro)toka lini ndugu wakagombana hazarani😢😢pole Sana

Haya yanajiri siku chache baada ya Rayvanny na mwanamuziki mwenzake, Harmonize, kuhusika kwenye vita mtandaoni kuhusu nani ni bora kuliko mwingine.

Ugomvi wa mtandaoni iliyovuta hisia za watumiaji wengi wa mtandao na mashabiki wa pande zote mbili.