Msije kushtuka mkisikia nimeimba kwa lugha ya Kichina - Diamond Platnumz

"Ahadi yangu iko palepale kuwa Mwaka huu ni nimeudtoa Maalum kwa ajili ya Muziki na kulinda kuwa Mnapata raha za kila aina."

Muhtasari

• Wimbo wake mpya wa 'Yatapita' unazidi kushika usukani katika majukwaa yote ya kupakuwa miziki tangu Ijumaa alipouachia.

Diamond adokeza kuimba Kichina
Diamond adokeza kuimba Kichina
Image: Instagram

Mwanamuziki Diamond Platnumz amesisitiza ahadi yake kwa mashabiki wake katika mwaka huu wa 2023 kuwa ni mwaka wa kuirejesha heshima yake kwa kuporomosha miziki mingi ya kuwakosha wote kama zamani.

Msanii huyo aliwataka masahbiki wake kukaa mkao wa kula na kusubiria akiwatumbuiza huku akisema kuwa watafurahi na kujihisi fahari kuwa naye katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Alisema kuwa katika harakati zake za kuachia miziki, huenda akalazimika kuimba kwa lugha ya Kichina, akiwataka mashabiki kutoshangaa pindi watakaposikia wimbo huo, huku akiwashukuru wote ambao wameendelea kutazama wimbo wake mpya ‘Yatapita’ na kuufanya kuwa kidedea katika majukwaa yote ya kupakua miziki ukanda wa Afrika Mashariki. Thank you for making “#Yatapia, wimbo nambari moja katika majukwaa yote 🙏🏼 .. Ahadi yangu iko palepale kuwa Mwaka huu ni nimeudedicate Maalum kwajili ya Muziki na kulinda kuwa Mnapata raha za kila aina! Msije kushtuka mkiskia nimeimba kichina huko,” Diamond alisema kwa utani.

Awali msanii huyo alisema wimbo huo unamkumbusha enzi akianza kutoka ngazi za chini ambapo alidokeza kuachwa kipindi hicho kutokana na kukosa riziki.

Alitumia fursa hiyo kuwashauri kina dada kutowapeza wanaume wao ambao wanachakarika kufanikisha maisha kipindi wanaanza kung’ang’ana.

Dada zangu, Kila Mwanaume anayempenda Mwanamke wake kwa dhati, jua kuwa anatamani ampatie kila hitaji lake…Anapochelewa kupata Usichoke kumvumilia na Kumkimbia, Muombee na kumpa Moyo ili kesho afanikishe kimaisha na Pamoja Muishi Maisha mliyoyatamani Muda wote….Msifanye kama Alonifanyiaga Sarah,” Platnumz alisema.

“Wimbo huu ukawatie Moyo na kuwafariji wote ambapo tunapitia changamoto mbalimbali za Kimaisha, InshaAllah Mwaka Huu Mwenyez Mungu atujaalie tuweze kufanikisha ndoto tuzipiganiazo.”