Diamond ajipata katika kashfa ya kuiba wimbo wa msanii wa Alikiba

Kashfa hii inakuja siku chache baada ya Diamond kuachia goma la 'Yatapita'

Muhtasari

• Vanilla ambaye amesainiwa chini ya lebo ya Kings Music alimtuhumu Diamond kwa kuiba mdundo na melody ya wimbo wake.

Msanii Vanilla amtuhumu Diamond kwa wizi wa wimbo
Msanii Vanilla amtuhumu Diamond kwa wizi wa wimbo
Image: Instagram

Kwa mara nyingine tena msanii Harmonize amekumbwa na tuhuma za kuiba mdundo na melody ya ngoma ya msanii mwingine katika wimbo wake mpya wa Yatapita.

Safari hii, dongo limerushwa kutoka kambi ya mpinzani wake mkuu, Alikiba.

Msanii Vanilla ambaye alisainiwa mwaka jana katika lebo ya Kings Music inayomilikiwa na Alikiba ameibuka na mapya akisema kuwa Diamond aliiba beat na melody ya ngoma yake ambayo aliitoa mwaka jana kama sehemu ya mpango wake wa kusainiwa Kings Music.

Vanilla kupitia instastories zake, aliandika kuwa ngoma yake ya Chizi ambayo ina miezi kadhaa sasa kwenye mitandao ya kijamii ndio yenye mdundo na melody halisia ambayo Diamond Platnmuz ametumia kwenye wimbo wake alioutoa mwishoni mwa juma lililopita kwa jina ‘Yatapita’

“Si mbaya lakini kukopy beat na melody inaonesha jinsi gani huu wimbo unaukubali na kuupenda kaka Asake, Ahsante,” Msanii huyo aliandika huku akiwataka mashabiki wake kuendellea kucheza wimbo wake wa Chizi kwa kuuradidi.

Hii si mara ya kwanza kwa Diamond kutuhumiwa kuiba sehemu za nyimbo za wasanii wenzake, kwani miaka michache iliyopita alituhumiwa kuiba mdundo wa ngoma ya Such Kinda Love yake Otile Brown akimshirikisha Jovial.

Pia mwaka jana kulikuwepo na madai kuwa msanii huyo aliiba wimbo wa msanii kutoka Nigeria, Asake na pia kuiba muonekano wa nywele zake, jambo lililowafanya Waswahili wengi kumbandika jina la majazi la ‘Asake wa Tandale’.