Jimal awashauri wanaume kuoa wake wanaomkimbilia Mungu lakini si wanaume

Kulingana na mfanyabiashara huyo, watu wanapaswa kutafuta suluhu kutoka kwa Mungu wanapokumbana na changamoto za ndoa.

Muhtasari
  • Wanawake wanapaswa kuepuka kutafuta wanaume wengine kwa sababu hii itasababisha uasherati na uzinzi
Mfanyabiashara Jimal Rohosafi
Mfanyabiashara Jimal Rohosafi
Image: Instagram//JimalRohosafi

Mfanyabiashara maarufu Jimal Rohosafi ana neno la ushauri kwa wanaume.

Amewataka wanaume kuoa wanawake wanaokimbilia kwa Mungu kutafuta msaada na si kwa wanaume wengine.

JImal na Amira walitengana baada ya kujihusisha na mwanasosholaiti Amber Ray.

Jimal anahudumu kama mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa Matatu jijini Nairobi. Amekuwa katika sekta ya matatu kwa miaka mingi ambapo alianza kama kondakta.

Kulingana na mfanyabiashara huyo, watu wanapaswa kutafuta suluhu kutoka kwa Mungu wanapokumbana na changamoto za ndoa.

Wanawake wanapaswa kuepuka kutafuta wanaume wengine kwa sababu hii itasababisha uasherati na uzinzi.

"Oa mwanamke anayemkimbilia Mungu mnapopatwa na matatizo lakini sio wanaume."

Chapisho hili kwenye mitandao ya kijamii liliibua maoni mengi kutoka kwa watumiaji wa mtandaoni.

Mashabiki wengi walikubaliana na maoni ya mfanyabiashara huyo.