Mungu azidi kuwapanua - Justina Syokau amwambia Natasha na mumewe

Syokau alisema kwamba Natasha na mumewe ni wazazi wake wa kiroho.

Muhtasari

• Nabii Carmel na mchungaji Natasha walikuwa wanasherehekea mwaka mmoja katika ndoa.

Syokau awatakia kila la kheri Natasha na mumewe
Syokau awatakia kila la kheri Natasha na mumewe
Image: Instagram

Mchungaji Lucy Natasha na mumewe Nabii Stanley Carmel wanasherehekea mwaka mmoja tangu waoane rasmi kama mke na mume.

Kupitia ukurasa wa Instagram, kanisa lao la ECC lilimuandikia ujumbe mzuri wa kuwatakia kila la kheri wanapofunga ukurasa wa mwaka mmoja na kupiga hatua kwenda ukurasa wa mwaka wa pili katika ndoa.

“Ndoa yanu ya kimungu iliyojaa upendo, urafiki na furaha imekuwa mfano wa kuigwa. Mmetutia moyo na kuonyesha upendo na ndoa bora zaidi. Tunasherehekea pamoja nawe siku hii maalum na tunakutakia miaka mingi zaidi iliyojaa furaha na furaha. Tunawatumia baraka na matakwa bora. Kwa maisha ya furaha pamoja mnapoendelea kuliongoza Taifa la Uwezeshaji Ulimwenguni!” kanisa lao liliwaandikia wapenzi hao ujumbe.

Aidha, msanii Justina Syokau, aliwaandikia ujumbe maridhawa kwenye ukurasa wake akiwataja kama wazazi wake wa kiroho.

Syokau alitumia kauli ya wimbo wake wa 2023 akiwatakia Mungu kuwapanulia mwaka wao katika maisha yao ya uchumba na huduma.

“Hongera sana wqazazi wangu wa kiroho, Mungu azidi kuwapanua mwaka wa 2023 uwe wa Baraka na mavuno tele. Nina furaha kwamba nyinyi ni wazazi wangu wa kiroho, nawapenda sana,” Justina Syokau aliandika.

Natasha na Carmel mwenye usuli wa India walioana mwaka jana katika hafla ya kifahari ambapo tangu hapo wamekuwa wakionesha mapenzi yao mitandaoni.

Wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, Carmel alidaiwa kumnunulia mkewe Natasha shamba la kifahari kama zawadi ya kuongeza mwaka mmoja kwenye rafu ya maisha yake.