Nimo Gachuiri azungumzia sakata la baby mama wa mumewe Mr Seed

Nimo alisisitiza kuwa bado anampenda Mr Seed licha ya sakata la kutoshughulikia mtoto wa baby mama wake.

Muhtasari

• Nimo alisema sakata hio huwa halimhusu na hana muda wa kulitia kichwani mwake.

Mr Seed na mkewe Nimo Gachuiri
Mr Seed na mkewe Nimo Gachuiri
Image: Instagram

Nimo Gachuiri, mke wa msanii Mr Seed kwa mara ya kwanza amezungumzia sakata la baby mama linalomzingira mume wake.

Mwanamke mmoja ambaye walizaa na msanii huyo katika siku za hivi karibuni amekuwa akimtupia makombo mitandaoni akisema msanii huyo hataki kusaidia katika malezo ya mtoto ambaye walizaa pamoja.

Wiki chache zilizopita wakati sakata hilo liliibuliwa na mwanadada huyo, Mr Seed hakutaka kabisa kulizungumzia huku akisema yeye alikuwa amezingatia muda wake mwingi katika mradi wake wa jumba la kifahari ambalo analijenga kwa ajili ya familia yake.

KIpindi hiki chote, Nimo hajawahi kuonekana akilizungumzia hilo lakini Jumatano kwa mara ya kwanza aliweka wazi ni kwa nini hataki kujihusisha na kujibizana kitandaoni na mwanamke anayedai kuzaa na mumewe.

“Mimi sitaki kujiingiza katika sakata hilo kwa sababu halinihusu, kwa njia hiyo mimi Amani ya akili yangu itakuwa sawa ndio maana sitaki kabisa kulizungumzia. Hilo sakata haliniudhi hata kidogo kwa sababu muda mwingi mimi najihusisha na mambo yanayonihusu,” Nimo alisema.

Nimo pia alisema kuwa mambo kama hayo yanayoendelea huwa hawayazungumzii na mpenzi wake Mr Seed.

“Mambo yenye hayanihusu, mimi na mume wangu tunajaribu kutoyazungumzia, kila mtu anashughulika na yake na tukifika kwa nyumba kila mmoja ako sawa. Hawezi kuwa anapigwa huko nje halafu pia akifika kwa nyumba ni mambo hiyo hiyo inaendelea, mapenzi hayajengwi hivyo,” Nimo alisema kwa upendo.

Alisema kuwa nyumbani ndiko kila mmoja anapata faraja baada ya kupigwa vita vya maneno huku nje siku mzima. Nimo alifutilia mbali dhana kuwa ni yeye tu anampenda Seed na kusema kwamba mapenzi yao yanaendana kwa kuwa hata yeye anampenda vile vile.

“Mapenzi katika ndoa ni kila mmoja kujitoa kwa mwingine, mmoja akichoka hakuna ndoa hapo. Wakati yeye ako sawa mimi siko vizuri, yeye ndio ananiinua, vile vile mimi nikiwa sawa nay eye hayuko sawa namuinua.hiyo ndio ndoa,” Nimo alisema kwa msisitizo kuwa anampenda Seed licha ya sakata hilo la baby mama.