Zuwena wa Diamond Platnumz asema ana miaka 17 tu!

Ni kama namba 17 ni namba ya bahati kwake, kutoka umri, inchi za runinga mpya hadi malipo aliyopata ya milioni 17 za Kenya.

Muhtasari

• Baadhi walionekana kupinga umri wake wakisema amepita hapo na yeye akakomalia kuwa ndio umri wake.

Mrembo Zuwena afunguka umri wake----17
Mrembo Zuwena afunguka umri wake----17
Image: Instagram

Recho Elias, mrembo aliyecheza kama mhusika mkuu kwenye video ya wimbo mpya wa msanii Diamond, Zuwena amezungumza kuhusu umri wake.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini Tanzania, Zuwena kama ambavyo ametambulika kutokana na maudhui ya wimbo huo kumzingira, anahoji kwamba wengi hawaamini anaposema bado ni tineja.

Mrembo huyo alifichua kwamba umri wake bado ni miaka 17 tu kwani hata kitambulisho cha taifa hana wala hajaruhusiwa kushiriki kwa baadhi ya mambo ya kijamii kwani kisheria yeye bado ni mtoto mdogo.

“Nina miaka 17 tu mimi, bado mbichi wewe unaonaje? Sasa unapinga kama wewe ndio umeiona kadi ya kliniki ama unataka nikutolee,” Mrembo huyo alijibu mtanagazaji ambaye bado alionekana kutoamini kuwa huo ndio umri wake halali.

Mrembo huyo pia alisema kuwa runinga ambayo ameinunua baada ya kupata mafanikio kutoka kwa umaarufu wa video ya Zuwena ni ya inchi 17, kitu ambacho kilifanya wengi kuhisi kwamba anakariri namba 17 tu kichwani mwake kwa kila kitu.

“Kila kitu kwake ni 17 tu,” mmoja alisema.

“Huyu mrembo ni Kamba namba 17 ni namba yake ya bahati kweli,” Kathryn Johnson alitania.

Katika mahojiano yake ya awali, Mrembo Zuwena alisema Diamond alimlipa kiasi cha shilingi milioni 17 za Kenya ili kushiriki kama mhusika Zuwena.

Hii 17 ina siri kubwa sana kwa mrembo Recho Elias!