Mchungaji adai atamfufua mwigizaji Kanumba, mamake amjibu kwa hisia kali

Mchungaji huyo aliibuka na madai haya wiki chache tu baada ya kuachiwa huru kutoka gerezani alikokaa kwa muda.

Muhtasari

• Akizungumzia suala hilo, mamake Kanumba alitokwa na machozi akisema kuwa kumbukumbu kama hizo zinaibua majonzi kwake.

• Kanumba alifariki miaka 11 iliyopita.

Mamake Kanumba ajibu Mfalme Zumaridi kumfufua mwanawe.
Mamake Kanumba ajibu Mfalme Zumaridi kumfufua mwanawe.
Image: Screengrab

Mchungaji mwenye utata nchini Tanzania, Mfalme Zumaridi ameibuka na jipya kuhusu kifo cha aliyekuwa mwigizaji nguli wa filamu za Kiswahili Steven Kanumba, wiki chache baada ya kufutiwac mashtaka yaliyokuywa yanamkabili.

Katika video moja ambayo mchungaji huyo wa kike alionekana akihubiri, anasikika akisema waziwazi tena kwa mbwembwe kwamba atamfufua Kanumba na kumrudisha hai.

“Mkimuona Steven Charles Kanumba, akitokea hivi, msishangae. Nimetangulia kuongea kweney vyombo vya habari,” Mflame Zumaridi alisema huku umati wa waumini wake ukishangilia kwa kiitikio cha “Amina!”

Video hiyo ilizua tafrani mitandaoni, baadhi wakisema kuwa Zumaridi anazidi kutafuta umaarufu kwa kurubuni akili za watu kumuamini kuwa ni binadamu mwenye uwezo uliopitiliza katika kufanya mambo.

Mamake Kanumba, Bi Flora Kanumba kwa uchungu mno alikemea matamshi hayo akisikitishwa kwamba mchungaji huyo anaweza kufikia hatua ya kufukuzia kiki kwa kifo cha mwanawe – jambo ambalo alisema linazidi kumuuma kwani watu hawataki kumuacha Kanumba kupumzika kwa Amani, miaka 11 tangu kifo chake.

“Tangu ameondoka hajawahi rudi, hata mitume na manabii waliokufa hawajawahi kurudi. Ina maana wewe unaye. Unaniumiza, tafuta kiki ingine, usitafute kiki na mwanangu mimi ndio ninaumia. Walisema Kanumba ni Freemason nikanyamaza, leo hii wameibuka na hili….” Mamake Kanumba alisema huku akiziidiwa na hisia.

Alimpa changamoto mhubiri huyo kuwafufua wengine akiwemo hayati Magufuli pamoja na mume wake anayesemekana kufariki pia miaka kadhaa iliyopita.

Alimpa Zumaridi makataa ya siku 7 ili kumuona mwanawe la sivyo sheria itachukua mkondo wake, huku akiomba pia serikali kumsaidia kudhibiti watu wenye kauli kama hizi ambazo zinaibua hisia za uchungu kufiwa na mwakawe aliyekuwa tegemeo lake.