Rotimi amsifia Vanessa Mdee kwa kumzalia mtoto wa pili chini ya miaka miwili

Wapenzi hao walitangaza kupokea mtoto wao wa kwanza mwezi Septemba mwaka 2021.

Muhtasari

• Rotimi alimsifia na kumtaja kama mtu ambaye ana uelewa mkubwa wa aina yake.

• Mdee alikuwa mpenzi wa muda mrefu wa Juma Jux kabla ya kutengana.

Rotimi akiwa na mke wake Vanessa Mdee.
Rotimi akiwa na mke wake Vanessa Mdee.
Image: Instagram

Msanii wa Marekani mwenye asili ya Nigeria Rotimi amemvisha koja maridadi la maua mpenzi wake Vanessa Mdee kwa kumzalia mtoto wa pili tangu watangaze upendo wao miaka michache iliyopita.

Takribani wiki moja iliyopita, Vanessa Mdee na Rotimi walitangaza kubarikiwa na mtoto wa pili na wiki moja baadae, bado Rotimi angali kuamini kwamba Mdee angemzalia mtoto wa pili kwa haraka hivo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rotimi alimsifia Mdee kwa kumuita Muhibu wake ambaye amesimama naye na kumpa sababu ya kutabasamu hata wakati anahisi kulemewa na mzigo mzito wa maisha.

Rotimi alidokeza kwamba alishuhudia moja kwa moja Mdee alijifungua na tukio hilo lilimfanya kuzidisha hata Zaidi mapenzi yake kwa mwanamuziki huyo mwenye sauti ya ninga kutoka Tanzania.

“Unapopitia Maisha na Kutafuta Mtu Ambaye Atatabasamu Pamoja Nawe Kupitia Aina Yoyote Ya Shida ... Unapopata Mtu Ambaye Kupitia Vikwazo Vya Aina Yoyote Bado Watapata Njia Ya Kucheka Na Wewe ... Hofu Inapozuka Silika Yao Ya Kwanza Ni Kunyakua Yako. Mkono Ili Nyote Mweze Kushiriki Ushujaa Wenu … JUA TU UMEMPATA RASMI MPENZI WAKO ️‍🔥” Rotimi aliandika kwenye picha hiyo ambayo pamoja na Mdee wako kwenye chumba cha leba.

Vanessa Mdee baada ya kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu Juma Jux miaka kadhaa iliyopita, alihamia Marekani ambapo alizama kwenye penzi zito na msanii Rotimi na muda si mrefu wakatangaza kuoana na kupata mtoto wa kwanza.

Chini ya miaka miwili, wapenzi hao tayari wamepata mtoto wa pili tena.