Andrew Kibe amshauri Xtian Dela kumblock mama yake kila mahali, " huyo si mama mzuri!"

"Mama, hii imezidi kwa kweli, huwezi enda mbali kiasi hicho kufukuza kiki mpaka kumtupa mtoto wako chini ya basi" Kibe alisema.

Muhtasari

• "Huyu mama ana lugha ya kuchagiza, ninaweza kuona ni kwa nini Xtian Dela hakutaka kuzungumza na yeye" - Kibe.

Kibe amtaka Dela kumblock mama yake kila mahali.
Kibe amtaka Dela kumblock mama yake kila mahali.
Image: Maktaba, Facebook

Mtetezi wa watoto wa kiume Andrew Kibe amemshauri mwanablogu wa YouTube Arthur Mandela Nyongesa almaarufu Xtian Dela kumblock mama yake kila mahali katika kile alisema kwamba mama huyo si mtu mzuri.

Kibe alitaja kitendo cha mama yake Dela kulia kwenye kamera kama kutafuta kiki, ikizingatiwa kuwa pia yeye ni muigizaji.

“Huyu ni mwanamke ambaye amekwenda kumuaibisha mtoto wake. Mama, hii imezidi kwa kweli, huwezi enda mbali kiasi hicho kufukuza kiki mpaka kumtupa mtoto wako chini ya basi. Sio vizuri, sasa ninaweza ona ni kwa nini Dela aliacha kukusikiliza. Kaka Dela, mblock kila mahali na utuonyeshe vile umemfungia kila mahali, huyo si mtu mzuri,” Andrew Kibe alisema.

Zogo la Xtian Dela na mama yake lilianza wiki jana ambapo mchungaji na mwigizaji Naomi Nyongesa alifanya mahojiano na blogu moja akimtuhumu mwanawe kwa kutotaka kuonana naye kwa miaka minne.

Mamake Dela alikuwa akiyazungumza hayo kwa uchungu baina ya misonyo na vilio, ishara ambayo Kibe ameitaja kama ya kuigiza na kumsuta vikali mchungaji huyo.

Kibe alisema kwamba wanawake si watu wazuri huku nje huku akisema kwamba hata yeye mama yake hajawahi muona binti yake wa miaka 8 sasa.

“Huyu mama ana lugha ya kuchagiza, ninaweza kuona ni kwa nini Xtian Dela hakutaka kuzungumza na yeye. Usifikirie wanawake ni wazuri huku nje, mimi mama yangu mpaka leo ameona binti yangu mara moja na ana miaka minane. Msifikirie kuwa watu ni wazuri, wewe ndio tu mzuri, kila mtu mwingine tu ni shetani,” Kibe alisema.