"Najivunia nilivyo!" Grand P asema kwa furaha baada ya kukutana na Ronaldinho Gaúcho

Grand P alisema kuwa alifedheheshwa katika uwanja wa ndege na maafisa wa polisi alipoenda kumpokea Ronaldinho.

Muhtasari

• Tazama vizuri tabasamu na furaha inayohuisha uso wa nguli huyo wa soka wa Brazil - Grand P.

• Grand P amekuwa gumzo la mitandaoni kwa muda mrefu kutokana na umbile lake la ajabu na kuchumbiana na mwanamke mnene kutoka Ivory Coast, Eudoxie Yao.

Grand P akiwa na Gaucho nchini mwao Guinnea.
Grand P akiwa na Gaucho nchini mwao Guinnea.
Image: facebook//Grand P

Wikendi iliyopita, aliyekuwa mchezaji maarufu wa soka kutoka Brazil, Ronaldinho Gaucho alikuwa katika ziara rasmi nchini Guinnea.

Mchezaji huyo mkogwe alikutana na msanii maarufu kutoka taifa hilo, Grand P, msanii ambaye amekuwa akigonga vichwa vya habari kutokana na umbile la mwili wake ambalo linamtoa kwa udogo wa kama mtoto vile licha ya kuwa na umri mkubwa ajabu.

Grand P kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii hakuweza kuificha furaha yake baada ya kukutana ana kwa ana na mkongwe wa soka Ronaldinho.

Grand P alikuwa miongoni wa wasanii maarufu walioalikwa pamoja na Gaucho na wengine kuhudhuria mechi murwa katika uwanja wa taifa hilo na hakusita kudokeza jinsi Gaucho alivyofurahi baada ya kukutana naye na kusalimiana.

“Watu wenzangu ambao walipaswa kulinda na kuheshimu taswira yangu walinifedhehesha, wakanidharau na kuachwa bila heshima katika chumba cha mapumziko cha watu mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ahmed Sekou Touré kwa ajili ya mapokezi ya #R10 kuwa mwakilishi mkuu wa utamaduni na marudio Guinea 🇬🇳 mkutano wa hadithi. Tazama vizuri tabasamu na furaha inayohuisha uso wa nguli huyo wa soka wa Brazil 🇧🇷 asante kwa kuzingatia na kumheshimu Ronaldinho Gaúcho 🙏🙏 Najivunia nilivyo,” Grand P alisema.

Grand P ambaye ni balozi wa utamaduni wa taifa hilo liilopo katika mwambao wa pwani ya Atlantiki Afrika Magharibi alidokeza kwamba alipofika katika uwanja wa ndege kumpokea Ronaldinho, alioneshwa kebehi na maafisa wa polisi lakini akasema baadae alipowa heshima ya kumpokea nguli huyo wa Brazili.

“Jioni njema kwa wote! Kama Balozi wa Utamaduni wa Guinea nilifedheheshwa leo kwa nguvu na afisa wa polisi na mawakala ambao walinidharau katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ahmed Sékou Touré.”

“Hata hivyo, nilialikwa na waandaaji kumkaribisha mwanasoka wa Brazil Ronaldinho. Kufukuzwa kutoka kwa chumba cha kupumzika cha VIP kama mtu mchafu anayejua hali yangu, kunidharau kama hivyo katika nchi yangu ni dharau kwangu na kwa Meneja wangu Alpha Sylla,” Grand P alilalama.