King Kaka amlimbikizia sifa mkewe huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa

Licha ya kumsherehekea alimlimbikizia sifa tele, kwa kuwa mke mwema na hata rafiki mwema.

Muhtasari
  • Kaka amemsifia mumewe kwa urembo wake wa kipekee na kuwa mama bora kwa watoto wao.
Image: INSTAGRAM// KING KAKA

Rappa maarufu King Kaka kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook amemsherehekea mkewe Nana Owiti kwa ujumbe mtamu.

Licha ya kumsherehekea alimlimbikizia sifa tele, kwa kuwa mke mwema  na hata rafiki mwema.

Katika ujumbe wake alimuahidi mkewe kuwa pamoja hadi nyakati zao za uzeeni.

Wawili hao wamekuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 5, na wamebarikiwa na watoto pamoja.

Kaka amemsifia mumewe kwa urembo wake wa kipekee na kuwa mama bora kwa watoto wao.

"Leo ni siku ya kuzaliwa ya rafiki yangu bora. Asante kwa kila kitu (unajua ninamaanisha) Mama mkubwa , Dada wa ajabu, Mpenzi mzuri wa moyo, Bibi mwenye busara, Ukuu, Mpishi wa kustaajabisha, Rafiki thabiti , Mzazi wa Kusudi, Mshangiliaji No 1, Gossip saa zingine, Urembo na Akili . Naweza kuomba nini zaidi? Heshima kufanya kitu hiki kinachoitwa maisha na wewe. Happy Birthday mke wangu kipenzi na May Happiness ikufuate na Mei matakwa yako yote yatimie. Hadi tukunje mgongo. Heri ya Siku ya Kuzaliwa Nana Owiti."