Guardian Angel ataka Wakenya kumtumia 'sadaka' kwa kufanya ombi la mvua kwa Mungu

"Huu wimbowa maombo ya mvua niliutoa wiki jana na Mungu amejibu, hebu wekeni hapo sadaka…” Guardian Angel

Muhtasari

• “Hili ndio ombi langu, kwa ajili ya nchi yangu, jua linawaka sana, mito inakauka Bwana….” Kionjo cha wimbo.

• Guardian Angel alikuwa kweney mtaa wa barabara moja katikati mwa jiji akinyeshewa wakati akirekodi video hiyo.

Guardian Angel awatanai Wakenya kumpa sadaka kwa ombi la mvua
Guardian Angel awatanai Wakenya kumpa sadaka kwa ombi la mvua
Image: Instagram

Mwenyekiti wa miziki ya injili Kenya wa kujitangaza mwenyewe Guardian Angel amewataka Wakenya kutoa dhabiu ya sadaka kwa kile alisema kwamba Mungu hatimaye amejibu maombi ya kuleta mvua.

Alhamisi asubuhi, sehemu nyingi za Kenya, haswa Nairobi, wakaazi waliamka na Baraka mfululizo za mvua nyingi ambazo zilianza kunyesha usiku wa Jumatano.

Angel alipakia video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na msanii mwingine wa miziki ya kidunia Dufla Diligon ambapo alitamba kwamba ni yeye alipiga mzuka wa kibao cha maombi kwa Mungu kwa ajili ya mvua – maombi ambayo yamejibiwa hatimaye.

Msanii huyo alikuwa kwenye mtaa mmoja wa barabara za katikati mwa jiji la Nairobi akiwa ananyeshewa na manyunyu ya mvua hizo.

“Toeni Sadaka Mungu amejibu maombi. Ni kama Mungu amekubali, ametukumbuka. Unaoan niliwapigia mzuka Fulani hapo wa maombi ya ajabu, sasa mvua ndio hizi. Haya sasa ndio yanaitwa maombi ya ukweli, unapiga ombi, Mungu anajibu. Si kupandisha watu mlima bure. Huu wimbo niliutoa wiki jana na Mungu amejibu, hebu wekeni hapo sadaka…” Guardian Angel alimaliza huku akitaja namba yake ya simu kwa utani.

Msanii huyo pia aliweka kionjo cha wimbo wake wa ‘Ombi Langu’, ambao alidai kuutoa wiki jana.

“Hili ndio ombi langu, kwa ajili ya nchi yangu, jua linawaka sana, mito inakauka Bwana….” Kionjo cha wimbo huo kilisikika kikiimba kwa umbali.

Mwezi jana, rais William Ruto kwa kushirikiana na watu mbali mbali wakiwemo wakenya na wasanii walikongamana katika uwanja wa michezo wa Nyayo katika kile walisema kuwa ni maombi ya kitaifa kuomba Mungu kushusha mvua.