Mwanahabari Lindah Oguttu alia baada ya kukosa katika orodha ya CAS wa rais Ruto

"Nitumieni sabuni nioge ka kurudi soko, ni kama pale kwa CAS kimeumana," - Oguttu alisema.

Muhtasari

• Mnamo Mei 2022, Lindah aliteuliwa kama mkuu wa sekretarieti katika kamati ya mpito ya Shirikisho la Soka la Kenya.

• Mwezi Februari, Oguttu aliwataka Wakenya kumuombea baada ya jina lake kuwa miongoni mwa majina 224 waliopendekezwa kuwania CAS.

Mwanahabari Lindah Oguttu alia kukosekana kwenye orodha ya CAS.
Mwanahabari Lindah Oguttu alia kukosekana kwenye orodha ya CAS.
Image: Facebook

Aliyekuwa mwanahabari wa runinga, Lindah Oguttu amezua utani kwenye mtandao wa Twitter baada ya kugundua kwamba alichunujwa kwenye orodha ya makatibu waandamizi katika wizara mbali mbali.

Orodha hiyo ya makatibu waandamizi ilitolewa Alhamisi alasiri na inajumuisha makatibu waandamizi 50.

Oguttu ambaye alionekana ni kama alikuwa ametarajia kwa hamu kubwa kupewa wadhifa miongoni mwa nafasi 50 zilizobuniwa na rais Ruto, alizua utani akitumia kauli ya ucheshi “kuoga na kurudi soko”.

“Ni kama pale CAS kimeumana. Wacha nioge nirudi soko. Tumeni sabuni mbio mbio mapema ndio best,” Lindah Oguttu aliandika.

Wiki chache zilizopita baada ya jina lake kupitishwa kwenye mchujo wa majina ya CAS waliokuwa wanawania nyadhifa 50, Oguttu aliwataka Wakenya kumuweka kwenye maombi kwani alikuwa ameona kabisa angekuwa miongoni mwa nafasi 50.

"Mkiamka kesho mtapatana na hii orodha. Naomba tupendane kama wakenya. Tafathali naomba muamke, mkunywe chai na mniombee. Maisha ni kuombeana tafadhali," alitweet.

Tume ya Utumishi wa Umma Mwezi jana ilitoa orodha ya watu 224 ambao waliorodheshwa kwa nyadhifa za CAS.

Mnamo Mei 2022, Lindah aliteuliwa kama mkuu wa sekretarieti katika kamati ya mpito ya Shirikisho la Soka la Kenya.

Akiwa na wanachama wengine 27, jukumu lake kuu wakati huo lilikuwa kusimamia masuala ya soka nchini kufuatia kuvunjwa kwa uongozi wa FKF uliokuwa unaongozwa na mwenyekiti Nick Mwendwa kwa madai ya ufisadi.

Muhula wake wa miezi sita ulipopita, Lindah alisema ilikuwa heshima kuhudumu katika FKF, akiongeza kuwa haukuwa uzoefu rahisi.