Chameleone:Bobi Wine ni miongoni mwa walionicheka upepo ulipoangusha jukwaa la shoo yangu

Chameleone alisema hakuamini kwani kitendo hicho kilikuwa kama usaliti, ikizingatiwa alilia wakati Wine alipigwa na polisi hadi kulazwa hospitali kipindi cha siasa.

Muhtasari

• Chameleone alisema alikuwa miongoni mwa watu waliosikitishwa na kupigwa kwa Wine kipindi cha siasa za mwaka 2021.

• Alinmtembelea hospitalini kumpa pole lakini Wine hakuhudhuria shoo yake ya Gwanga Mujje.

Jose Chameleone amshtumu Bobi Wine kwa kumcheka jukwaa la shoo yake liipoanguka.
Jose Chameleone amshtumu Bobi Wine kwa kumcheka jukwaa la shoo yake liipoanguka.
Image: Instagram

Msanii wa Uganda wa muda Jose Chameleone amedhibitisha kuhusu ugomvi wake na msanii aliyegeuka kuwa mwanasiasa Bobi Wine.

Chameleone katika mahojiano ya vyombo vya habari hivi majuzi alisema kwamba alikuwa anamheshimu sana mwanasiasa huyo wa upinzani n ahata kipindi kimoja alipojeruhiwa wakati wa rabsha za siasa, Chameleone alilia kwa tukio hilo.

Lakini wakati jukwaa la shoo yake ya Gwanga Mujje lilipoangushwa na tufani kubwa mnamo Februari 10 kusababisha kuahirishwa kwa tamasha hilo hadi Februari 24, Bobi Wine alikuwa mmoja wa watu waliozua ucheshi na utani kuhusu tukio hilo la kimbunga na mvua kali kuangusha jukwaa.

"Wakati jukwaa langu lilipoanguka, niliona marafiki ambao walikuja," Chameleone alisema katika mahojiano na vyombo vya habari. "Watu walisema mambo mengi, lakini sikujibu, lakini niliona walichokisema."

Msanii huyo wa ‘Badilisha’ alikumbuka wakati Wine aliachwa akiwa amejeruhiwa baada ya ugomvi na maafisa wa usalama huko Arua wakati wa joto la kisiasa.

Chameleone alisema ni miongoni mwa waliomtembelea katika Hospitali ya Nsambya licha ya kuwa hawakuwa karibu wakati huo.

Pia alidai kuwa haikuwa hatua ya kisiasa kwa sababu wakati huo hakuwa amemwomba tikiti ya NUP. Chameleone alionyesha nia ya kuwania umeya wa Kampala katika uchaguzi wa 2021.

"Alipopigwa huko Arua, sikuwa na uhusiano wowote naye wakati huo. Na sitaki tufanye hili kisiasa kwa sababu sikuwa nimemwomba tikiti ya chama," alisema.

"Lakini kwa kujua historia yetu na jinsi alivyojitahidi katika tasnia ya muziki pamoja, nilipewa mamlaka ya kwenda Nsambya... Na nilipofika huko, nililia. Nilijua alikuwa amepigwa ngumi zaidi ya uzito wake."

Aliongeza: "Sitamlaumu, lakini nitakuwa wazi kwake, lazima tuondoe maringo kwenye baadhi ya mambo haya. Kuna kile wanachoita huruma. Nikiwa na au bila yeye, ilibidi nifanye shoo yangu.”

 

"Wala silalamiki... ukimuuliza atakuambia kwanini hakuweza kuja... namkumbusha tu kwani atanifanya nini?... alipata matatizo, tulikuwa na wasiwasi... Hata Pallaso alimtembelea kwa sababu hiyo. Hata baba yangu.”