Vera Sidika na Amber Ray watupiana mabomu kisa nani wa kwanza kutumia Helikopta

Vera Sidika alimtuhumu Amber Ray kwa kumuibia wazo la kutumia Helikopta kudhihirisha jinsia ya mtoto wake ajaye.

Muhtasari

• Vera Sidika alisema kwamba alikuwa wa kwanza kuja na wazo la kutumia helikopta kudhihiridha jinsia ya mtot wake kabla ya Ray kuiga.

• Ray alimjibu akimwambia kwamba si wazo lake bali ni la mwanamke kwa jina Jenna Karvunidis aliyefanya hivyo 2008.

Vera Sidika na mber Ray wapigana kisa nani wa kwanza kuja na wazo la kutumia helikopta
Vera Sidika na mber Ray wapigana kisa nani wa kwanza kuja na wazo la kutumia helikopta
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Vera Sidika kwa mara nyingine tena amemsakama kooni mwanafasheni Amber Ray katika kile anasema kwamba Ray anajaribu kumuiga kwa kila kitu, haswa katika suala ya kudhihirisha jinsia ya mtoto wao mtarajiwa na Kennedy Rapudo.

Sidika alianzisha vita hiyo kupitia Instastories zake akisema kwamba hafla ya wiki moja iliyopita ya Ray na Rapudo kudhihirisha jinsia ya mtoto wao ilikuwa ni wazo lake katika kutumia ndege aina ya helikopta.

Wikendi iliyopita, Amber Ray alionekana kwenye helikopta pamoja pia na kuweka bango kubwa barabarani kutangaza hafla ya kudhuhirisha jinsia ya mtoto wake mtarajiwa.

Kaitka suala la kutumia helikopta, Vera Sidika alisema ni wazo lake ambalo alilifanya mwezi Desemba bila watu wengi kujua na hivyo kumtuhumu Amber Ray kwa kumuibia wazo lake hilo.

“Kama malikia, napenda sana kuwahimiza watu kusema kweli, pia wao walikuwa wanataka kudhihirisha jinsia ya mwanao kwa kutumia helikopta, mpaka pale nilipopakia yangu na ikatrend kwa siku tatu mitqandaoni. Baada ya hapo, walilazimika kutafuta njia mbadala kwa sababu wangetumia chopper ingeonekana kawaida sana kuwa wameniiga,” Sidika alisema kwa sehemu.

Alizidi kusema kwamba Amber Ray asingeweza kuahirisha matumizi ya helikopta kwa sababu tayari alikuwa ameshaikodisha na ilibidi aitumie tu kudhihirisha jinsia ya mtoto wao.

“Aliambia mtu aliyekuwa anasimamia mipango yake kwamba alikuwa anataka kuiga kila kitu nilichokifanya katika kudhihirisha jinsia ya mtoto wangu. Na alitaka kuifanya kabla yangu kwenye runinga, ili wakati yangu itakapofanyika, iwe kwamba ni mimi nimemuiga. Uovu ni mwingi sana katika hii dunia,” Vera Sidika alisema.

Sidika alizidi kusema kwamba Amber anamchukia sana na kumuita ghushi na mwenye roho mbaya lakini wakati huo huo anazidi kumfuatilia na kutaka kuiga kila kitu anachokifanya.

“Nimejifunza kitu kimoja kwamba wabaya wako ni mashabiki wako ambao hawataki kukubali. Hakuna kitu kibaya katika kumhimiza mtu lakini ni vizuri wakati himizo hilo linakuja kutoka kwa sehemu nzuri. Na mimi siombi radhi katika hili kusema kweli,” Sidika alisema.

Kwa upande wake, Amber Ray alimwandikia ujumbe mrefu wa kumtaka kumkoma akisema kwamba wazo la kudhihirisha jinsia ya mtoto si la Mkenya yeyote bali wote wanaliiga kutoka kwa mwanamke mmoja kwa jina Jenna Karvunidis aliyefanya hivyo mara ya kwanza mwaka 2008.

Alisema kwamba wote wanafanya dhihirisho la jinsia ya watoto wao wajao si kuwaonehsa watu kitu bali kujiridhisha wenyewe.

“Tunafanya karamu ili kufurahiya isiwe mtindo bora mitandaoni. Mchezo wangu ni wa asili, umaarufu wangu huja kwa kawaida ... kama vile ulivyofanya sasa. Kuwa mbunifu kufurahiya sio kuburudisha. Hebu starehe yako iwe burudani yao… Na Unikome tafadhali!!!” Amber Ray alijibu mipigo.