"Nitakuwa rais wa kwanza kutoka Luo Nyanza" Jalang'o apuuzilia mbali Raila kuwa rais

Jalang'o alisema sababnu yake yqa kwenda kwa Ruto ikulu ni kujifunza jinsi ya kushinda uchaguzi, sababu Ruto hajawahi shindwa.

Muhtasari

• “Nilienda kwa Ruto kujifunza ujuzi wa kushinda uchaguzi kwa sababu Ruto hajawahi kushindwa" - Jalang'o.

RAIS WILLIAM RUTO NA MBUNGE WA LANG'ATA FELIX ODUOR
Image: JALANG'O/TWITTER

Kuna video ambayo inasambaa mitandaoni kwa wiki kadhaa sasa na ambayo haijulikani ni lini haswa ilirekodiwa.

Video hiyo ni ya mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor almaarufu Jalang’o alifunguka kwa mapana sababu zake za kukutana na rais William Ruto wiki kadhaa zilizopita katika ikulu ya Nairobi.

Katik video hiyo, Jalang’o anasema kwamba yeye bado ni mwanafunzi wa kisiasa na lengo lake kuu kukutana na Ruto ni kujifunza jinsi ya kuwa rais, akijipiga kifua kwamba ana uhakika atakuwa mtu wa kwanza kutoka Luo Nyanza kuwa rais – na hivyo kupuuzilia mbali uwezekano wa Raila Odinga kuwa rais mbele yake.

Jalang'o alisema ukweli kwamba Ruto hajawahi kushindwa katika uchaguzi ulimsogeza karibu naye ili kuchukua mikakati yake na njia anazoweza kujipanga kuwa mkuu wa taifa.

“Nilienda kwa Ruto kujifunza ujuzi wa kushinda uchaguzi kwa sababu Ruto hajawahi kushindwa uchaguzi tangu aingie katika siasa. Nilienda kujifunza jinsi yeye (Ruto) amekuwa akiipata sawa iwe ni kuiba au kwa njia nyinginezo. Nawambia ninapata ujuzi huo na najua nitakuwa mtu wa kwanza kutoka jamii ya Wajaluo kuwa rais. Mtakumbuka kauli ninayowaambia leo wakati kijana kutoka eneo bunge la Gem anatangazwa kuwa rais,” Jalang’o alisema.

Wiki jana katika hafula ya Betty Kyallo kuzindua maeneo mapya ya saluni yake, Jalang’o aliwaambia wanahabari kwamba angekuwa katika maandamano ya Raila Odinga Jumatatu ya Machi 20 licha ya kufukuzwa katika mkutano wa Maanzoni Machakos, lakini siku mbili baadae alijiunga na wabunge wenzake kutoka Luo Nyanza ambao walimtembelea Ruto ikuluni kukiri kwamba hatakuwa miongoni mwa watakaokuwa kwenye maandamano hayo.