Ukipata mimba nitakufungia ndani na kukufanyia kila kitu - Wolper amwambia Sepetu

Mwigizaji Wema Sepetu kwa muda mrefu amekuwa akionesha uchu na tamaa kuu ya kuzaa mtoto wake na kuitwa mama.

Muhtasari

• Wema alikuwa ametoa angalizo kwamba hakuwa bado amepata mimba bali ni kipindi tu watu walimuona wakadhani ameshajibiwa ombi la muda mrefu.

Wolper aweka ahadi kwa Wema atakapopata mimba
Wolper aweka ahadi kwa Wema atakapopata mimba
Image: Instagram

Mwigizaji mkongwe Jacqueline Wolper amemwandikia mwigizaji mwenza Wema Sepetu akimwambia kwamba siku atapata ujauzito, atakuwa mtu wa kwanza kujitolea na kumfungia ndani akimhudumia kwa kila kitu ilmradi asiteseke kipindi chote cha ujauzito.

Wema Sepetu alikuwa amechapisha angalizo akisema kwamba hakuwa na ujauzito bali ni kipindi tu watu waliona mahali akiigiza kuwa ni mjamzito.

Sepetu ambaye amekuwa akionesha nia na tamaa kubwa ya kupata angalau mtoto wake naye siku moja alisema kwamba hakuwa na ujauzito na ikitokea siku moja atapata mimba wala hatomueleza mtu yeyote kwani itakuwa siri yake.

“Angalizo..!!! Kile ni kipindi... bado mimi sina ujauzito...!!! Na hata kama nikishika mnahisi nitasema kweli...?🤔🤔 Yaani ndo ile Mungu kasema, "Sasa acha nikubariki tumbo lako Wema" , halafu PAAP "MIMBA"... Sisemi Ng'o...!!! Ila Naitamani jamani...🤦🏼‍♀️🤦🏼‍♀️🤦🏼‍♀️ Tuseme Inshallah... â€œ Wema Sepetu aliweka wazi.

Hata hivyo, mashabiki wake wengi walimtakia kila la kheri katika hilo ombi lake la muda mrefu na Wolper alikuwa mmoja wa wale waliweka nadhiri naye kwamba siku atapata mimba basi yeye atajitolea kumfanyia kila kitu.

“Ishallah Baby yani Nitakuwa wa kwanza kukufungia ndani Nakukuletea utakacho Binadamu si watu Mungu atakupa katika jina la Yesu rafiki yangu,” Wolper alisema.

Wolper ni rafiki wa muda mrefu wa Wema na yeye tayari ni mama wa watoto wawili ambapo mwaka jana amekamilisha kheri kwa kufunga ndoa ya kanisani kabisa na Rich Mitindo.

Katika chapisho linguine, Wema alipakia picha kama yuko kwenye dimbwi la mawazo vile na kusema kwamba anawaza sana siku atapata mtoto na awe wa kiume halafu anayemfanana riale kwa ya pili.