Nilipoteza wafuasi milioni 11 Instagram chini ya saa 24 Ronaldo aliponiacha - Ex wa CR7

Baada ya kuachana na Ronaldo, aliwatishia wafuasi wake kuacha kumfollow kama walijihisi, na kwa mshangao alipoteza zaidi ya milioni 11.

Muhtasari

• Mwanamitindo mkuu Irina Shayk, 37, na nyota wa Al-Nassr Ronaldo, 38, walichumbiana kati ya 2010 na 2015.

• Muda mfupi baada ya kuachana na Ronaldo, Irina alianza kuchumbiana na nyota wa Hollywood Bradley Cooper.

Aloiyekuwa mpenzi wa Ronaldo afunguka kupoteza wafuasi milioni 11 Instagram baada ya kuachana naye
Aloiyekuwa mpenzi wa Ronaldo afunguka kupoteza wafuasi milioni 11 Instagram baada ya kuachana naye
Image: Instagram

Nyota wa usakataji kabumbu kutoka Ureno Christinao Ronaldo ni staa mwenye maisha ya fasheni ya kipekee, jambo ambalo limemvutia warembo wengi katika maisha yake, kabla ya kukutaka na mke wake wa sasa Georgina Rodriguez.

Lakini mmoja amefunguka kupoteza wafuasi Zaidi ya milioni 11 kwenye ukurasa wake wa Instagram chini ya saa 24 tu baada ya kuachana na Ronaldo.

Mwanamitindo mkuu Irina Shayk, 37, na nyota wa Al-Nassr Ronaldo, 38, walichumbiana kati ya 2010 na 2015.

Raia huyo wa Kirusi alikutana na Ronaldo alipokuwa ametoka tu Manchester United kwenda Real Madrid mwaka 2009. Lakini walichukua muda wao na hawakuanza kwenda nje kwa mwaka mwingine.

Wawili hao walikaa pamoja kwa miaka mitano baada ya kuwa wanandoa namba moja wa soka.

Walakini, mambo yaliisha mnamo 2015 kwa madai ya kutokubaliana juu ya kuanzisha familia pamoja.

Taarifa zaidi zinadai Irina alikataa kwenda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa mama mpendwa wa Ronaldo.

Hii ilikataliwa na Irina, ambaye alisema kupitia mwakilishi: "Amekuwa karibu na familia yake wakati wote wa uhusiano wao. Uvumi wowote mbaya kuhusu Irina na familia ya Ronaldo ni uongo kabisa, na haujawa kuwa sababu ya kuvunja uhusiano wao.”

Muda mfupi baada ya kuachana na Ronaldo, Irina alianza kuchumbiana na nyota wa Hollywood Bradley Cooper. Na mwaka 2016 Ronaldo alikutana na mpenzi wake sasa Georgina Rodriguez.

Mrembo huyo aliambia jarida moja kwamba Mwaka huo huo, aliwaambia mashabiki wake kwenye Instagram waache kumfuata ikiwa "wanamjua tu kama mpenzi wa zamani wa Cristiano Ronaldo."

Kwa kushangaza, wafuasi wa Irina walipungua kwa 11m ndani ya masaa 24 tu - hasara ya asilimia 75 ya wafuasi wake.

Kusonga mbele hadi 2023 na Irina sasa ana watu milioni 21 wanaomfuata kwenye Instagram.

Lakini ex wake Ronaldo yuko mbele kwa maili nyingi akiwa na wafuasi milioni 564 - zaidi ya mtumiaji mwingine yeyote kwenye jukwaa la mtandao huo wa kijamii.

Irina sasa anasemekana kuwa single baada ya kutengana na Cooper mnamo 2019.