Nyce wa Njeri na mpenzi wake Galvin Leting wanazidi kutamba na ujauzito wao, woki tano baada ya kufichua kutarajia mtoto pamoja.
Wa Njeri alipakia picha ya pamoja na mpenzi wake na kusema kwamba ujauzito huo si suala la kuficha kwani Mungu mwenyewe aliamua kwamba ni sharti uonekane na kila mtu, kila mahali aendapo.
Kulingana na mwigizaji huyo, ujauzito wake ni kama Baraka ambapo haifichiki hata kidogo.
“Hii ni baraka moja yenye Mungu alikataa kuficha π₯π₯π₯..... Alisema popote utaenda kila MTU anajua uko Na Baraka,” Nyce wa Njeri alisema.
Msanii huyo aliwatakia wafuasi wake kheri na Baraka ya Mungu kuwatiririkia wazi wazi kama ambavyo mimba yake inaonekana wazi pasi na kufichika.
“Maombi yako yajibiwe hadharani ndio Mungu aoneshe umaarufu wake Na wewe π. Mwamini Mungu atakuvusha katika hayo yote.... Ana uwezo kuliko kitu kingine chochote π. Wewe ni baraka katika jina la Yesu... Amina?” wa Njeri alitoa himizo.
Wiki tano zilizopita, wapenzi hao walitangaza ujauzito wao ambapo Wa Njeri anatarajia mtoto wa pili. Walitangaza ujauzito wao kupitia video ya wimbo waliouita ‘Kwako Nyumbani’
Baadaye, mwigizaji huyo wa zamani wa Auntie Boss alishiriki picha ya mimba yake kwenye Instagram akiwa kando ya mpenzi wake. Picha hizo zilivutia jumbe nyingi za pongezi kutoka kwa mashabiki wao mtandaoni.