Thee Pluto atangaza kuwania useneta 2027, mwezi baada ya kudokeza kuondoka mitandaoni

Mwanablogu huyo wa YouTube mwenye umri wa miaka 23 alidokeza hilo katika chapisho akiwa shambani kwake.

Muhtasari

• ” Seneta 2027✔” alinukuu picha aliyopiga akiwa kwenye shamba lake la nguruwe.

• Tangazo hili linakuja mwezi mmoja tu baada ya kudkeza kwamba ifikapo mwisho wa mwaka huu ataondoka mitandaoni kabisa.

Thee Pluto atangaza kuwania useneta 2027.
Thee Pluto atangaza kuwania useneta 2027.
Image: Instagram

Mtayarishaji maarufu wa maudhui kwenye YouTube Robert Ndegwa Kamau almaarufu Thee Pluto atajiunga na siasa mwaka wa 2027.

Pluto aliweka tangazo hilo kwenye instastory yake akiweka picha moja iliyomuonesha shambani na panga mkononi na kuandika kwamba yeye ni seneta katika uchaguzi ujao wa mwaka 2027.

” Seneta 2027✔” alinukuu picha aliyopiga akiwa kwenye shamba lake la nguruwe.

Hakutoa maelezo zaidi kuhusu chapisho hilo. Thee Pluto hata hivyo huenda akawania kiti cha useneta kaunti ya Nakuru ikizingatiwa kwamba alizaliwa Naivasha.

Hata hivyo, wengi wanaambatanisha chaoisho hilo na lile ambalo kijana huyo wa miaka 23 alimwambia mpenzi wake Felicity Shiru siku chache nyuma akisema kwamba amechoka na maisha ya mitandaoni na huneda akatathmini kuachia ngazi katika mitandao ya kijamii.

Pluto ambaye umaarufu wake ulitokana na kipindi cha ‘Loyalty Test’ kwenye mtandao wa YouTube hata hivyo katika siku za hivi karibuni hajakuwa akionekana kupakia klipu hizo, jambo ambalo limewatia mashabiki wake tumbo joto kuwa huenda anamaanisha kile alichosema kuwa ameanza kuwa mchache mitandaoni.

“Nimeanza kuhisi mitandao ya kijamii si kitu changu. Polepole, ifikapo mwisho wa mwaka huu au mwaka ujao, kwa mapenzi ya Mungu, nitaacha mitandao ya kijamii, nitafute vishikizo vyangu na kuishi maisha ya faragha. Kweli video ya mwisho itakuwa ni mimi kufuta vishikizo vyangu. Wakati mwingine unachoka na kuhitaji akili lakini ukiwa na hizo mpini, najua nitarudi huko,” alimwambia mpenzi wake Felicity.

Kando na kuwa mwanablogu wa YouTube, Pluto ambaye ni baba wa mtoto mmoja na Shiru amekuwa akijihusisha na ukulima wa nguruwe, ambapo mara kwa mara imekuwa kama biahsara yake kwenye machapisho ya kila siku Instagram.

Azma yake ya kujiunga katika siasa inakuja mwaka mmoja tu baada ya kudaiwa kuzawadiwa gari la kifahari na mwanasiasa wa kike Wangui Ng’ang’a.