logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pascal Tokodi na Grace Ekirapa wamzawadi binti yao wa miezi 11 runinga kwenye chumba chake

Mwezi jana katika kusherehekea miezi 10 ya kuzaliwa, walimzawadi midoli ya thamani.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 April 2023 - 09:41

Muhtasari


  • • Chumba cha AJ pia kina sakafu ya zulia ya kijivu ambayo mamake alisema ilikuwa ya kuongeza joto.
  • • Pia waliongeza fanicha yenye droo zinazoweza kufungwa ambazo alisema ni mahali ambapo wanahifadhi vifaa vya kuchezea vya AJ.
Ekirapa na mumewe Tokodi wamzawadi mtoto wao wa miezi 11 na runinga

Wanandoa Pascal Tokodi na Grace Ekirapa wamepandisha viwango vya hadhi ya aina yake kwenye chumba cha binti yao AJ.

Mwigizaji huyo na mkewe mwanahabari walikuwa wanasherehekea miezi 11 ya kuzaliwa kwa mwanao na walifanya mabadiliko makubwa katika chumba chake.

Wawili hao walipakia video kwenye YouTube yao wakionesha jinsi wamerekebisha na kusasisha chumba cha mwanao ikiwemo kupakwa rangi upya na kumuongezea runinga ya kujivinjari kwa vipindi avipendavyo vya watoto.

Chumba hicho kina ukuta wenye picha za wanyama na Ekirapa alieleza kuwa hakutaka kumlazimisha binti yake rangi kwa vile watu wengi wangepaka rangi ya waridi ikiwa wangekuwa na binti.

Runinga bapa iliyowekwa ukutani na Grace alieleza kuwa atakuwa akiitumia kucheza nyimbo za mbelezi au nyimbo za kuabudu za ala ili kumsaidia AJ kupata usingizi.

Chumba cha AJ pia kina sakafu ya zulia ya kijivu ambayo mamake alisema ilikuwa ya kuongeza joto ndani ikilinganishwa na sakafu ya maroon ya awali ambayo haikuwa na vigae.

Pia waliongeza fanicha yenye droo zinazoweza kufungwa ambazo alisema ni mahali ambapo wanahifadhi vifaa vya kuchezea vya AJ na Grace aliongeza kuwa ataibadilisha kuwa rafu ya vitabu wakati binti yake atakuwa na umri wa kutosha kuelewa kazi za vitabu.

Katika kusherehekea miezi kumi ya kuzaliwa mwezi jana, wanandoa hao walimnunulia binti yao bidhaa ghali kama midoli ya kuchezea ya gari, baiskeli na vitu vingine vyenye thamani kubwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved