Andrew Kibe: Akothee mimi ndio rafiki yako pekee nakuambia ukweli hiyo 'make-up' uliharibu!

“Ni kama mtu aliyefanyiwa ubandikizaji wa kichwa maana rangi ya ngozi ya uso na shingo hazikuwa zinaendana hata kidogo," - Kibe.

Muhtasari

• Kibe pia alikejeli picha ya Akothee akisema kuwa mwanamuziki huyo alikuwa anakaa kama maiti.

• Kibe alisema kuwa alitumia muda mwingi sana kujaribu kujizuia kutosema maneno hasi kwa harusi ya Akothee lakini ilishindikana.

Andrew Kibe amkejeli Akothee kwa make up yake siku ya harusi
Andrew Kibe amkejeli Akothee kwa make up yake siku ya harusi
Image: Screengrab//YouTube

Mwanablogu wa YouTube, Andrew Kibe kwa mara nyingine ameshusha mijeledi kwa wale walioshiriki katika kumpendezesha mwanamuziki Akothee siku ya Jumatatu katika tukio kubwa la harusi yake na mzungu Mr Omosh.

Kibe kupitia podikasti yake ya kila siku, alimweka Akothee kwenye kikaango kama kawaida yake na kumsuta vikali kwa kuvalishwa ‘make-up’ ambayo alisema haikuendana hata kidogo na rangi ya ngozi yake, ikimfanya kuonekana uso kama maiti.

“Kutoka juzi nimeona picha na video nyingi kutoka kwa harusi ya Akothee. Macho hayaoni tena. Nimeona vitu vingi mpaka nikajiuliza Mungu wangu nitapona kweli. Niliangalia nikaona amevaa’ make-up nikasema, watu hamko wakweli. Kuna picha moja niliona nikasema picha hiyo ikiwekwa kwa mlazo, anakaa kabisa mtu amekufa. Sijui pengine ni jua la Kenya,” Kibe alisema.

Kibe alisema kuwa msanii huyo hakuwa na marafiki wazuri wanaomtakia mema, kwani angekuwepo rafiki mzuri angemshauri kuwa hiyo ‘make-up’ haijamkaa sawa na badala yake kumtaka kukoma kuitumia na kuwa halisia.

Kibe alijitapa kuwa ndiye rafiki wa kweli pekee kwa Akothee na ndio maana aliamua kumwambia ukweli bila kubakisha akiba ya maneno yake.

“Kutoka kwa kile niliona nilisema walimkosea. Kwani hakuna mtu hata mmoja katika marafiki zake ambaye angemuambia wewe si mtu wa make-up, wewe ni mtu wa ‘lip balm’ peke yake. Kuna shida ya rangi ya ngozi kutofanana na hiyo –make-up’.”

“Ni kama mtu aliyefanyiwa ubandikizaji wa kichwa au nini. Akothee nataka ujue kwamba huna marafiki wa kweli, kama ungekuwa nao, wangekuambia ukweli. Mimi tu ndiye rafiki wako wa kweli. Nitafute, njoo nikueleze,” Kibe alisema.

Kibe alisema kuwa alitumia muda mwingi sana kujaribu kujizuia kutosema maneno hasi kwa harusi ya Akothee lakini baada ya kuona picha hizo, ilimbidi tu kutema nyongo.

Jumatatu, Akothee alifanya harusi ya kifahari na mpenzi wake Mzungu kutoka Uswidi, harusi ambayo ilihudhuriwa na watu mashuhuri mbalimbali kutoka wanasiasa hadi maceleb wa matabaka mbalimbali.