Mkongwe wa Ohangla ataja makosa yatakayommaliza Prince Indah Kimuziki kwa haraka!

"Msanii yeyote anayefanya kazi ya usanii lazima ajieshimu kwanza sababu magonjwa ni mengi," - Tony Nyadundo alishauri.

Muhtasari

• Tony Nyadundo, mkongwe wa Ohangla ambaye alitumbuiza kwenye harusi ya Akothe alisema wanamuziki wachanga wanajimaliza haraka kwa kupenda wanawake.

• "Kama yeye anaenda kwa mganga ajisaidie anaganguliwa kivingine shauri yake" - Tony Nyadundo.

Nyadundo amshauri Indah jinsi ya kudumu kwenye muziki.
Nyadundo amshauri Indah jinsi ya kudumu kwenye muziki.
Image: Facebook, Twitter

Msanii mkongwe wa miziki ya Kijaluo ya Ohangla Tony Nyadundo ametaja tofauti kubwa iliyopo baina ya wasanii wa zamani na wa kisasa huku pia akimtaja Prince Indah kama msanii wa Ohangla ambaye anaweza kufanya vizuri.

Nyadundo hata hivyo alisema kuwa Indah kuna makossa makubwa ambayo anayafanya na huenda yakamgharimu vibaya sana katika safari yake ya muziki.

“Prince Indah anaweza akafnaya vizuri lakini sasa makossa anayofanya, unajua wimbo ni kama hatimiliki, ukitoa wimbo leo halafu tena kesho mashabiki wakuambia toa wimbo mwingine, wanakumaliza…. Utafikiri wanakupenda kumbe safari yako katika muziki inaendelea kufupishwa. Ushauri wangu ni kwamba wimbo ukiwa mzuri unaweza ukasikilizwa hata miaka 10,” mzee wa kazi alisema.

Nyadundo ambaye alikuwa msanii wa kipekee kualikwa na Akothee kutumbuiza kwa njia spesheli katika harusi yake alisema kuwa wasanii wa zamani miziki yao ina mafunzo chanya kwa jamii tofauti na miziki ya kisasa ambayo ujumbe wao mara nyingi ni mbaya na unaoeneza usherati.

Nyadundo alishauri wasanii wa sasa kujiheshimu na kutia bidii kimuziki, akisema kuwa hakuna njia ya mkato ya kufanikiwa kama kwenda kwa mganga na vitimbi vingine.

“Mtu yeyote anayefanya anavyotaka ni shauri yake. Kama yeye anaenda kwa mganga ajisaidie anaganguliwa kivingine shauri yake. Mimi nafaamu kwamba msanii yeyote anayefanya kazi ya usanii lazima ajieshimu kwanza sababu magonjwa ni mengi. Katika usanii kuna pilkapilka za kupanda na kushuka, huwezi mfananisha mtu mwenye talanta na mwenye anayeenda kufunzwa usanii. Mwenye talanta hudumu kwa muda mrefu,” Nyadundo alisema.

Msanii huyo japo hakufichua kima alichojizolea kutoka kwa kuwa mtumbuizaji wa kipekee katika harusi ya Akothee, alisema alipokezwa kitita kizuri tu cha kumwezesha kufanikisha maisha yake.