Mafanikio ninayoyapata sasa hivi niliyafanyia kazi, sikusaidiwa na mtu - Vera Sidika

Sidika alikanusha dhana kwamba mafanikio na utajiri alio nao sasa hivi alisaidiwa na mtu.

Muhtasari

• "Ni mimi mwenyewe niliyejisukumia mwenyewe kwa bidii yangu,” Vera Sidika alisema.

• Sidika ni mmoja wa wanasosholaiti matajiri zaidi nchini Kenya.

Vera Sidika akosoa wale wanaodhani mafanikio yake alisaidiwa na mtu.
Vera Sidika akosoa wale wanaodhani mafanikio yake alisaidiwa na mtu.
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Vera Sidika amenyoosha maelezo kuhusu dhana nyingi zinazozunguka utajiri wake mkubwa, haswa baada ya Amber Ray kudai kuwa yeye ndiye anayemlea mume wake Brown Muazo.

Sidika anasema kuwa kinyume na jinsi watu wengi wanavyofikiria kuwa mafanikio yake alisaidiwa na mtu kuyapata, yeye anajua jinsi alichakarika na kujibidiisha hadi kufika hapa alipo sasa.

“Watu wanafikiri kwamba milango yote imefunguliwa mbele yangu nilisaidiwa na mtu, lakini jua unajua nini? Ni mimi mwenyewe niliyejisukumia mwenyewe kwa bidii yangu,” Vera Sidika alisema.

Mwanasosholaiti huyo mstaafu anatajwa kuwa miongoni mwa wasanii matajiri Zaidi wa nchini Kenya, kutokana tu na kufanya kazi za usosholaiti – na kujifungulia biashara zake kutokana na mapato ya kazi hiyo.

Baadhi ya watumizi wa Instagram walikubaliana na yeye wakisema kuwa kuna wengine wanaona mtu amefanikiwa na kujua kwamba kama si kusaidiwa basi huenda alitumia njia za mkato.

“Nukuu inasema kila wakati lazima usukuma mlango peke yako ili mambo yafanye kazi na sio kungoja hadi mlango ufunguke kwa sababu utabaki nje,” mmoja alisema.

“Mitazamo ya watu ni nyingi sana, lakini mradi unajua ni bidii yako, hakuna baya,” mwingine alisema.

Sidika wiki chache zilizopita alipapurana vikali mitandaoni na Amber Ray baada ya kudai kwamba Ray aliiba mawazo yake ya kudhihirisha jinsia ya mwanawe kwa kutumia ndege aina ya helikopta.

Sidika alimsuta vikali Ray akisema kuwa wazo hilo lilikuwa lake na yeye ndiye alikuwa wa kwanza kufanya ‘gender reveal’ kwa helikopta.

Wawili hao walizidiha ugomvi mpaka Ray kusema kuwa ana uwezo wa kumfadhili mume wa Sidiki, Brown Mauzo.

Sidika kwa sasa ni mjamzito na wanatarajia mtoto wa pili pamoja na mwanamuziki Brown Mauzo baada ya kuanza kukaa pamoja mwaka 2021.

Ni mmoja kati ya wanawake mashuhuri waliochaguliwa kuigiza kwenye kipindi cha uhalisia cha Real Housewives of Nairobi ambacho kinapeperushwa kwenye Shomax.