Milly Wajesus kutokea bila malipo kama mpambe kwa harusi ya wapenzi mabikira

Milly pia alisema wanandoa hao mabikira ni lazima wawe tayari kufunga na kuomba na yeye mlimani kwa siku 21.

Muhtasari

• Milly anasema haya siku chache tu baada ya kuzomewa kwa kutaja bei ghali kwa watakaotaka huduma zake kama mpambe kwenye harusi.

• Alitetea mwaliko kuwekwa miezi 6 kabla kwa sababu atakuwa yuko bize sana kufanya maombi na wanandoa wengine.

Milly Wajesus atangaza kutokea bila malipo kwa harusi za mabikira.
Milly Wajesus atangaza kutokea bila malipo kwa harusi za mabikira.
Image: Instagram

Siku chache baada ya kufana kama mpambe kwenye harusi ya Akothee, mwanablogu Milly Wajesus sasa anadai kuwa yuko tayari kutoa huduma za upambe bila malipo kwa harusi zingine.

Hii inakuja siku tatu tu baada ya kushambuliwa na kukejeliwa mitandaoni alipoweka chapisho kuhusu bei zake kwa maharusi watakaotaka huduma za mpambe.

"Sasa nina kadi ya bei ya kuwa kwenye foleni yako (Telezesha Kushoto Kuona Kadi ya Kadiri) Ninapata maswali mengi sana kuhusu kuwa kwenye safu ya watu kwa hivyo tafadhali angalia viwango vya slaidi za mwisho na uwasiliane," Milly aliandika.

Milly katika chapisho lake la Ijumaa alasiri, alisema kuwa sasa yuko tayari kutoa huduma za upambe kwa maharusi wapya bila malipo lakini akatoa masharti mawili ambayo lazima maharusi hao watimize.

Mwanablogu huyo anayeigiza katika kipindi cha uhalisia cha Oh Sisters alisema kuwa maharusi hao sharti wawe wote mabikra na pia wawe tayari kufunga naye mlimani kwa wiki tatu.

Watu wamejitetea sana kwa DM yangu na pia kwenye barua pepe kuhusu bei zangu katika kutokea kama mpambe kwenye harusi. Nimeamua kufanya BILA MALIPO. Hii ni ofa ya kipekee kwa maharusi ambao wako tayari kufunga na kuomba mlimani pamoja na mimi kwa siku 21 na ni lazima wote wawe bikra,” Milly alisema.

Kando na masharti hayo makuu mawili, Milly pia alisema kuwa ni lazima apewe mwaliko miezi sita kabla, akisisitiza kwamba harusi na ndoa inayojengwa kwa misingi ya Mungu kamwe haivunjiki.

“Pia inabidi unipangie angalau miezi 6 mapema maana nitakuwa busy kuomba na wanandoa wengine. Ndoa iliyoanzishwa na Mungu itastahimili jaribu la wakati,” Milly Wajesus alisema.

Milly alikuwa mmoja wa wanawake waliokuwa kama wapambe katika harusi ya mwanamuziki Akothee Jumatatu Aprili 10 ambapo alifunga ndoa ya kifahari na Mswizi Mr Omosh.