Hiba Abouk, mke wa Achraf Hakimi avunja kimya, "nilihitaji muda wa kutafakari mshtuko huu!"

"Ni kweli kwamba, nikiwa na watoto wawili, ni ngumu kihisia, lakini mimi si wa kwanza na sitakuwa wa mwisho,”

Muhtasari

• "Jambo muhimu ni kwamba nina amani ya akili kwa kuwa nimejaribu na kufanya kila kitu nilichopaswa kufanya." - Abouk.

• "Nilihitaji muda kutafakari mshtuko huu.”

Mke wa Hakimi amevunja ukimya kufuatia sakata la talaka na kukosa mali.
Mke wa Hakimi amevunja ukimya kufuatia sakata la talaka na kukosa mali.
Image: Twitter

Mke wa zamani wa beki wa PSG, Achraf Hakimi, Hiba Abouk hatimaye amevunja ukimya huku akifichua kuwa alikuwa akipata nafuu kutokana na mshtuko huo.

Kumbuka kwamba Hakimi na mkewe, Hiba Abouk walitengeneza vichwa vya habari wakati mahakama ilipofichua kwamba Hakimi hakuwa na mali yake kwa jina lake ila ya mama zake.

Kulingana na Hiba Abouk, alikuwa mtulivu kuhusu hali hiyo licha ya mashtaka ya ubakaji dhidi ya Hakimi, akiongeza kuwa alihitaji muda ili kutafakari mshtuko huo.

Akizungumza na ELLE katika mazungumzo yaliyofanywa kwa lugha ya Kihispanyola na kutafsiriwa, Abouk alisema, “Sijambo. Kuna siku ambazo ni kama hii, na zingine ambazo lazima ujue jinsi ya kupiga makofi na kufanya maamuzi, wakati mwingine magumu, na kuzoea hali mpya. Nani angefikiria kwamba pamoja na kukabili maumivu ya kawaida ambayo kutengana kunahusisha na kukubali huzuni ambayo kushindwa kwa mradi wa familia ambao nilikuwa nimejitolea mwili na roho kunahusisha, ningekabiliana na aibu hii. Nilihitaji muda kutafakari mshtuko huu.”

"Unapojitenga, unarekebisha maisha yako, lakini sio kitu maalum pia: lazima uchukue funzo kutoka kwa suala hilo. Ni kweli kwamba, nikiwa na watoto wawili, ni ngumu kihisia, lakini mimi si wa kwanza na sitakuwa wa mwisho,” alisema.

Kulingana na tafsiri na mazungumzo hayo, Abouk alisema kuwa alijaribu kadri ya uwezo wake lakini mumewe alikuwa na nia nyingine ya kudoea nje. Alibainisha kwamba angalau ameshapata Amani ya nafsi na tulizo la akili.

"Jambo muhimu ni kwamba nina amani ya akili kwa kuwa nimejaribu na kufanya kila kitu nilichopaswa kufanya. Kuna maamuzi ambayo hayawezi kufanywa mara moja. Kwangu mimi ni msingi wa kutokimbilia wakati wa shida.”

Abouk na Hakimi wana watoto wawili, Amín, 3, na Naim, 1, pamoja. Wawili hao walioa mnamo 2020, miaka miwili baada ya kukutana mnamo 2018.